NBA: Golden State Warriors Waweka Rekodi Baada Ya Kufungwa Tena

28th October 2019

OKLAHOMA, Marekani- Timu ya mpira wa kikapu ya Golden State Warrior wameingia kwenye rekodi mbaya baada ya kufungwa kwa vikapu 120-92 ikiwa ni kwenye mchezo wa pili mfululizo safari hii ikiwa ni dhidi ya Oklahoma City Thunder.

OKC vs GSW
OKC vs GSW
SUMMARY

Kufungwa mara mbili kwenye mechi za mwanzo wa msimu inakuwa ni historia kwao kwani mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Warriors ambao walikuwa ni wababe kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo wakiingia fainali mara zote hizo na kuchukuwa taji mara tatu wamejikuta wakilambishwa mchanga na Thunder ikiwa ni siku chache tangu walipotoka kufungwa na LA Clippers.

Kuondoka kwa Kevin Durant ambaye alijiunga na Brookly Nets mara baada ya kumalizika msimu pia kumkosa Klay Thompson aliyemajeruhi kumewafanya Warriors wabaki na tegemeo moja tu ambalo ni nyota Stephen Curry.

Hata hivyo mambo bado hayajakuwa mazuri kwa nyota huyo huku eneo la ulinzi la timu hiyo likionekana kuwa ndiyo tatizo kubwa kwasasa.

Kwenye mchezo dhidi ya Clippers, timu hiyo iliruhusu kufungwa vikapu 141 na mchezo wa leo alfajiri wamefungwa tena vikapu 120 wakifanya jumla ya vikapu 261 ndani ya mechi mbili.

Mbali na hilo lakini pia wameingia kwenye rekodi ya kuwa na tofauti kubwa ya idadi ya alama za kufunga na kufungwa ikiwa kwasasa wana -47.

Kufungwa mara mbili kwenye mechi za mwanzo wa msimu inakuwa ni historia kwao kwani mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Kwenye mchezo wa leo alfajiri Dennis Schroder wa Thunder amefunga vikapu 22 na kuwa nyota kwa upande wa timu yake ambayo imeibuka na ushindi.

Curry yeye alifunga vikapu 23 kwa upande wa Warriors lakini hata hivyo havikuwa na msaada kwenye upande wa matokeo.

Matokeo Kamili

Golden State Warriors 92-120 Oklahoma City Thunder

Charlotte Hornets 101-120 Los Angeles Lakers

Brooklyn Nets 133-134 Memphis Grizzlies (OT)

Portland Trail Blazers 121-119 Dallas Mavericks

Miami Heat 109-116 Minnesota Timberwolves

Imeandaliwa na Badrurin Yahaya