NBA: Golden State Warriors Wapoteza Mchezo Wao Wa 8 Msimu Huu

10th November 2019

CALIFORNIA, Marekani- Hali ya timu ya Golden State Warriors inazidi kuwa mbaya ndani ya ligi ya NBA baada ya alfajiri ya leo tena kukubali kipigo cha 114-108 kutoka kwa Oklahoma Cuty Thunder.

Golden State Warriors
Golden State Warriors
SUMMARY

Mapengo ya wachezaji wao nyota bado yanawagharimu Warriors ambao walianza msimu bila ya Kevin Durant aliyehama huku wakimkosa Klay Thompson ambaye ni majeruhi kwa msimu mzima.

Danilo Gallinari amefunga vikapu 19 huku Dennis Schroder akifunga vikapu 18 wote wao kwa upande wa Oklahoma. 

Naye Chris Paul aliongeza vikapu 16 pamoja na asisti 9 huu Steven Adams akifunga mara 13.

Nyota kwa upande wa Warriors alikuwa ni D'Angelo Russell aliyefunga vikapu 30 ambavyo vilikuwa ni vingi kulinganisha na wachezaji wengine kwenye mchezo huo. Alec Burks aliongeza 23 lakini bado hawakuwezesha kuipesha timu yao na kipigo hicho cha nane msimu huu.

Mapengo ya wachezaji wao nyota bado yanawagharimu Warriors ambao walianza msimu bila ya Kevin Durant aliyehama huku wakimkosa Klay Thompson ambaye ni majeruhi kwa msimu mzima.

Stepehn Curry amevunjika mkono wiki iliyopita atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu huku Draymond Green akikosekana kwa mechi za hivi karibuni kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.

Matokeo Mengine:

Dallas Mavericks 138-122 Memphis Grizzlies

Houston Rockets 117-94 Chicago Bulls

Boston Celtics 135-115 San Antonio Spurs

Golden State Warriors 108-114 Oklahoma City Thunder

New Orleans Pelicans 115-110 Charlotte Hornets

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya