NBA: Golden State Warriors Kukosa Huduma Ya D'Angelo Russell Kwa Wiki Mbili

17th November 2019

CALIFORNIA, Marekani- Mwaka wa tabu: Hivi ndivyo unaweza kusema ukiwaongelea Golden Sate Warriors ambapo taarifa zimetoka kuwa watakosa huduma ya mchezaji wao D'Angelo Russell kwa kipindi cha takribani wiki mbili.

D'Angelo Russell
D'Angelo Russell
SUMMARY

Alifanyiwa uangalizi wa awali kwenye mkono wake lakini alishindwa kurejea uwanjani kuendelea na mchezo. Kwa mujibu wa vipimo vya X-Ray inaonesha kuwa hajavunjika ila tu misuli baadhi ilishtuka.

Russell alishindwa kuendelea na mchezo wakati timu yake hiyo ilipopokea kichapo kutoka kwa Boston Celtic siku ya Ijumaa baada ya kuonekana kugongana na Daniel Theis.

Alifanyiwa uangalizi wa awali kwenye mkono wake lakini alishindwa kurejea uwanjani kuendelea na mchezo. Kwa mujibu wa vipimo vya X-Ray inaonesha kuwa hajavunjika ila tu misuli baadhi ilishtuka.

Russell ambaye kwa msimu huu ana wastani wa kufunga alama 24, assisti 6.7 kwa kila mchezo alimaliza mechi hiyo akiwa na alama 12 na asisti 7.

Kukosekana kwa Russell kwenye mechi kadhaa zijazo kunaongeza idadi ya wachezaji wa GSW waliokuwa nje kwasababu za majeruhi.

Klay Thompson hajacheza mechi hata moja na hatarajiwi kucheza mechi yeyote msimu huu. Sambamba na huyo pia mchezaji wao nyota zaidi Stephen Curry alivunjika mkono wa kushoto kwenye mechi za awali msimu huu na atakuwa nje walau hadi mwezi Desemba.

Wengine walioko nje ni Kevon Looney, Jacob Evans, na Alen Smailagic ambao wanasumbuliwa na majeraha.

Alfajiri ya kuamkia kesho Golden State watakuwa tena uwanjani kucheza dhidi ya New Orleans Pelicans.

Hadi hivi sasa Warrios wameshacheza mechi 13 msimu huu ambapo wameshinda mechi 2 na kufungwa michezo 11.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya