NBA: Giannis Aiongoza Milwaukee Bucks Kuinyoosha Houston Rockets

25th October 2019

MILWAUKEE, Marekani -MVP wa msimu uliopita wa ligi ya NBA, Giannis Antetokounmpo amefunga vikapu 30, assisti 11 na kufanya rebound 13 wakati akiiongoza timu yake ya Milwaukee Bucks kuiubuka na ushindi wa 117-111 dhidi ya Houston Rockets

Giannis Antetokounmpo
Giannis Antetokounmpo
SUMMARY

Mbali na Giannis lakini pia Wesley Matthews alifunga vikapu 14 huku pia Ersan Ilyasova akifunga alama muhimu ikiwemo ile ambayo ilipindua meza kwenye robo ya tatu na kuwafanya Bucks kuanza kuongaza kwa 91-90.

MILWAUKEE, Marekani -MVP wa msimu uliopita wa ligi ya NBA, Giannis Antetokounmpo amefunga vikapu 30, assisti 11 na kufanya rebound 13 wakati akiiongoza timu yake ya Milwaukee Bucks kuiubuka na ushindi wa 117-111 dhidi ya Houston Rockets kwenye dimba la Toyota Center.

Hata hivyo ilimlazimu Giannis kumalizia mchezo huo akiwa nje baada ya kufanya faulo kwa mara ya sita na hivyo kutolewa nje zikiwa zimesalia dakika 5:18 huku timu yake ikiwa inaongoza kwa 101-95.

Wachezaji wenzake walipambana kuhakikisha hakuna kinachoharibika na hadi mchezo unafika mwisho Bucks wakawa wamerekodi ushindi wao wa kwanza wa msimu.

Mbali na Giannis lakini pia Wesley Matthews alifunga vikapu 14 huku pia Ersan Ilyasova akifunga alama muhimu ikiwemo ile ambayo ilipindua meza kwenye robo ya tatu na kuwafanya Bucks kuanza kuongaza kwa 91-90.

Eric Bledsoe, Khris Middleton na Brook Lopez wote walifunga alama 11 na Pat Connaughton alifunga alama zake 10 na kufanya pia rebound 11.

Kwa upande wa Rockets, Russell Westbrook alifunga vikapu 24, assisti 7 na alifanya rebound 16 kwenye mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na miamba hao.

James Harden alifunga vikapu 19 na assisti 14 huku Clint Capela akimaliza mchezo kwa kufunga alama zake 13.

Matokeo ya Mchezo Mwingine

Atlanta Hawks 117-100 Detroit Pistons


Imeandaliwa na Badrudin Yahaya