NBA: Celtics Wasalimu Amri Mbele Ya Bunduki Za Kawhi Leonard Na Paul George

21st November 2019

BOSTON, Marekani- Kitu ambacho kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa LA Clippers kimetimia baada ya alfajiri ya leo kuwashuhudia wachezaji wawili nyota Paul George na Kawhi Leonard wakicheza timu moja kwa mara ya kwanza.

Kawhi Leonard
Kawhi Leonard
SUMMARY

Kwenye mchezo dhidi ya Celtics ambao ulikuwa ni mkali sana hasa ukilinganisha ubora wa vikosi vyote viwili, Lou Williams ndiye aliyeibuka shujaa kwa upande wa Clippers baada ya kufunga alama 27 huku George akiongeza 25 na asisti 8.

Wachezaji hao wamecheza kwenye mchezo dhidi ya Boston Celtics ambapo Clippers wameibuka na ushindi wa 107-104 kwenye muda wa nyongeza (OT).

Nyota hao wote wawili walisajiliwa mwanzo wa msimu lakini George hakuanza kukitumikia kikosi hicho mapema kutokana na majeruhi huku Kawhi yeye akiwa amecheza michezo kadhaa msimu huu.

George aliporudi uwanjani kwenye michezo minne iliyopita, Kawhi naye alikuwa nje kwa majeraha ya enka kitu ambacho kilifanya wasikutane uwanjani.

Hata hivyo kwenye mchezo wa leo, George akiwa ndani Kawhi naye amepona na amerejea kikosini kuungana na wenzake.

Kwenye mchezo dhidi ya Celtics ambao ulikuwa ni mkali sana hasa ukilinganisha ubora wa vikosi vyote viwili, Lou Williams ndiye aliyeibuka shujaa kwa upande wa Clippers baada ya kufunga alama 27 huku George akiongeza 25 na asisti 8.

Kawhi yeye kwa upande wake alifunga alama 17 huku Patrick Beverley akifunga alama 14 kwa upande wa Clippers.

Jayson Tatum amefunga alama 30 ambapo ni rekodi yake bora kwa msimu huu. Marcus Smart amefunga 15 na asisti 8, Brad Wanamaker amefunga 14 na Kemba Walker amefunga alama 13 wote hao kwa upande wa Celtics.

Matokeo Mengine

Boston Celtics 104-107 LA Clippers (OT)

Houston Rockets 95-105 Denver Nuggets

Utah Jazz 103-95 Minnesota Timberwolves

Golden State Warriors 94-142 Dallas Mavericks

Milwaukee Bucks 135-127 Atlanta Hawks

New York Knicks 104-109 Philadelphia 76ers

Orlando Magic 97-113 Toronto Raptors

Charlotte Hornets 91-101 Brooklyn Nets

Cleveland Cavaliers 100-124 Miami Heat

Detroit Pistons 89-109 Chicago Bulls

San Antonio Spurs 132-138 Washington Wizards

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya