NBA: Anthony Davis Afunga Vikapu 40, Lakers Wakiisambaratisha Memphis Grizzlies

30th October 2019

LOS ANGELES, Marekani- Nyota wa LA Lakers, Anthony Davis amefunga vikapu 40 na kufanya rebound 20 ndani ya dakik 31 wakati akiisaidia timu yake kuisambaratisha Memphis Grizzlies kwa jumla ya vikapu 120-90.

Anthony Davis
Anthony Davis
SUMMARY

LOS ANGELES, Marekani- Nyota wa LA Lakers, Anthony Davis amefunga vikapu 40 na kufanya rebound 20 ndani ya dakik 31 wakati akiisaidia timu yake kuisambaratisha Memphis Grizzlies kwa jumla ya vikapu 120-90.

Naye LeBron James aliongeza vikapu vyake 23 wakati akichagiza ushindi huo kwa upande wa Lakers ambao wameshinda mchezo wa tatu mfululizo.

Grizzlies ambao walipata wakati mgumu sana hasa ilipofika robo ya tatu waliongozwa Ja Morant ambaye alifunga vikapu 16, Jonas Valanciunas 14 na Grayson Allen aliyefunga vikapu 13.

Lakers wamemka vizuri na kushinda michezo yao mitatu mfululizo tangu walipokumbana na kipigo kwenye mchezo wa kwanza tu wa ufunguzi dhidi ya jirani zao LA Clippers.

Ushirikiano wa Davis na LeBron unaendelea kushika kasi na kama wengi walivyotabiri kwamba huenda msimu huu timu hiyo ikawa moto wa kuotea mbali hasa kwenye safu yao ya ushambuliaji.

Matokeo Mengine

Memphis Grizzlies 91-120 Los Angeles Lakers

Atlanta Hawks 97-112 Miami Heat

Dallas Mavericks 109-106 Denver Nuggets

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya