Muda Wa Mikeka: EPL Kuondoka Na Vichwa Vya Makocha Wawili Wikiendi Hii?

30th November 2019

LONDON, Uingereza- Ligi kuu ya soka ya Uingereza inaendelea kwa mechi sita kupigwa kwenye viwanja tofauti ambapo vigogo 12 vitashuka kugombea alama 3 muhimu.

Marco Silva
Marco Silva
SUMMARY

Upo tayari kushinda MAMILIONI leo?

Bet mechi kali za leo kupitia SportPesa bila kutumia bando lako ujishindie MAMILIONI kwa JERO au zaidi.

Bofya HAPA kubet sasa

Mechi ambazo zitafuatiliwa kwa hamu kwa siku ya leo na kesho ni mbili ambazo zimebeba hatma ya makocha Manuel Pellegrin wa West Ham na Marco Silva wa Everton.

Tofauti na Silva ambaye yeye kesho atakuwa ugenini dhidi ya Leicester City, huenda hatma ya Pellegrin ikajulikana mapema zaidi kwani leo atakuwa ugenini na kikosi chake cha West Ham kucheza dhidi ya Chelsea.

Bila shaka uvumilivu wa mabosi wa West Ham dhidi ya Pellegrin utaishia wikiendi hii endapo atapigwa kwa mara nyingine tena na kwa dalili zinavyoonesha kipigo kipo.

Chelsea v West Ham

Hii ni mechi ya mzunguko wa 14 kwa kila timu ambapo Chelsea wanaonekana kuwa vizuri sana kuliko wapinzani wao West Ham ambao gari bado haijawaka.

West Ham wapo nafasi ya 17 wakiwa na alama zao 13 wakati Chelsea wao wakiwa nafasi ya nne na alama zao 26.

Chelsea wanaingia kwenye mechi ya leo wakiwa hawajashinda kwenye michezo yao miwili iliyopita ya michuano yote wakati West Ham wao hawajashinda kwenye michezo 8 iliyopita. Mara yao ya mwisho kushinda ilikuwa ni Septemba 22 walipo wafunga Man United 2-0.

Timu hizi kabla ya mchezo wa leo zimeshakutana mara 46 ambapo Chelsea wanaongoza kwa kushinda mara 25 huku West Ham wakishinda mara 12. Mechi 9 zimekwisha kwa sare.

Katika mechi zao tano walizokutana hivi karibuni Chelsea wameshinda mara mbili, West Ham wameshinda mara moja na mechi mbili zimekwisha kwa sare.

Liverpool v Brighton

Vinara wa ligi kuu ya Uingereza ambapo Liverpool leo watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kucheza dhidi ya Brighton.

Ni aina ya mchezo ambao huwezi kuona namna ya Majogoo hao kupoteza hasa ukizingatia rekodi yao dhidi ya Brighton kwa misimu miwili mfululizo.

Kwenye mechi nne ambazo wamekutana kwenye historia ya EPL, Liverpool wameshinda michezo yote kwa kufunga jumla ya mabao 11 huku Brighton wakifunga bao moja tu.

Liverpool ambao hawajafungwa hadi sasa wameshinda michezo yao minne mfululizo iliyopita huku Brighton wakiwa wamefungwa mara tatu na kupata ushindi mara mbili kwenye michezo yao mitano iliyopita.

Tottenham v Bournemouth

Kocha Jose Mourinho leo atakuwa ndani ya dimba la White Hart Lane kuiongoza Spurs kwa mara ya kwanza kwenye uwanja huo kwa michezo ya ligi ya Uingereza.

Alipewa kibarua wiki iliyopita na kazi yake ya kwanza ilikuwa ugenini hivyo leo atapata fursa ya kukaribishwa na mashabiki wa nyumbani kwake atakapo kabiliana na Bournemouth.

Spurs wana rekodi nzuri dhidi ya Bournemouth wakiwa wameshinda michezo 6 kati ya 8 ambayo wamewahi kukutana kwenye historia ya EPL.

Bournemouth wao wameshinda mara moja na sare baina ya wababe hao ni moja tu kwenye michezo hiyo waliyokutana.

Michezo yao mitano ya hivi karibuni kukutana Spurs wameshinda mara 4 lakini Bournemouth wanashikilia rekodi ya kushinda kwenye mchezo wao wa mwisho walipokutana.

Newcastle United v Man City

Mabingwa watetezi wa EPL baada ya kutoka kuwapiga Chelsea leo watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Newcastle kwenye mchezo wa mapema zaidi wa EPL leo.

Mchezo huu utakuwa ni wa 39 kwa timu hizo kukutana. Kwenye michezo 38 iliyopita Man City ni wababe wa Newcastle wakiwa na rekodi ya ushindi mara 23 dhidi ya 8 huku sare baina yao zikiwa ni 7 tu.

Man City wameshinda mechi 3 kati ya tano zilizopita huku mechi moja ikiisha kwa sare. Newcastle wao wanajivunia kushinda mechi ya mwisho walipokutana kwenye uwanja huo Septemba mwaka jana.

Wenyeji Newcastle hawana mwendo mzuri wakiwa wanasusua kwa kushinda mechi mbili kati ya tano za mwisho huku wakiwa wamefungwa mara mbili na sare moja.

Wao Man City wameshinda mechi nne na kufungwa mechi moja katika mechi zao tano za EPL zilizopita.

Mechi Nyingine Leo

Burnley v Crystal Palace

Southampton v Watford

Imeandaliwa na Jerry Mlosa