Mkwasa "Atuma Salamu" Kwa Wapinzani, Yanga Ikiitandika Ndanda Ugenini

9th November 2019

MTWARA, Tanzania- Timu ya soka ya Yanga leo wakiwa ugenini wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ndanda.

Patrick Sibomana
Patrick Sibomana
SUMMARY

Mabadiliko hayo madogo yameleta tija kwani Sibomana ndiye aliyefunga bao la pekee kwenye mchezo huo mnamo dakika ya 75 kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya eneo la boksi.

Ushindi huo ni watatu mfululizo kwa Yanga kwenye ligi kuu bara msimu huu huku kwa mara ya kwanza wakicheza bila ya aliyekuwa kocha wao Mwinyi Zahera.

Kaimu kocha mkuu wa Yanga leo aliwaanzisha kikosini wachezaji Patrick Sibomana, Rafael Daud na Jafar Mohamed ambao wamekuwa hawachezi kwa kipindi cha hivi karibuni.

Mabadiliko hayo madogo yameleta tija kwani Sibomana ndiye aliyefunga bao la pekee kwenye mchezo huo mnamo dakika ya 75 kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya eneo la boksi.

Mchezo huu ni watatu mfululizo kwa Yanga kupata ushindi msimu huu. Baada ya kuanza kwa kufungwa kisha sare, Yanga waliwafunga Coastal Union na Mbao na kwenye mechi zote hizi wachezaji wamelamba posho ya shilingi milioni 10 kutoka kwa msambazaji rasmi wa jezi zao, kampuni ya GSM.

Yanga sasa wamejiondoa mkiani mwa ligi baada ya kufikisha alama 10 huku wakiwa wameshuka dimbani mara 5, wakati Ndanda wataendelea kubaki huko na alama zao 7 baada ya mechi 9.

Hii ni mara ya pili kwa Yanga kushinda kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona tangu timu hiyo ilipopanda daraja misimu mitano iliyopita. Mara ya mwisho kupata ushindi ilikuwa ni msimu wa 2017-18 ambapo walishinda kwa 2-1.

Matokeo Mengine

KMC 1-2 Kagera Sugar

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya