Mida Ya Mikeka: Arsenal Leo Watatokea Wapi Mbele Ya Leicester City?

9th November 2019

LEICESTER, Uingereza- Ligi kuu ya Uingereza inaendelea leo kwa michezo 6 kupigwa kwenye viwanja tofauti. mchezo ambao utavuta hisia za wengi ni ule ambao utawakutanisha Leicester City ambao watakuwa nyumbani kuwaalika Arsenal.

Arsenal FC
Arsenal FC
SUMMARY

Upo tayari kushinda MAMILIONI leo?

Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi kali za leo kupitia SportPesa ujishindie MAMILIONI kwa JERO au zaidi.

Bofya HAPA kubet sasa

Mchezo huo utakuwa na mvuto wa aina yake hasa kutokana na uimara wa timu zote mbili kwasasa.

Ni jambo la wazi kabisa kwamba Leicester wapo vizuri sana msimu huu ukilinganisha na Arsenal ambao bado wanayumba kupata matokeo.

Huu ni mtihani mwingine mgumu kwa kocha Unai Emery ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wa Arsenal ambao hawaridhishiwa na mwenendo wa timu yao.

Hata hivyo kuelekea mchezo wa leo Arsenal wanabebwa na rekodi yao ya muda wote ambapo kwenye michezo 26 waliyocheza, Washika Bunduki hao wameshinda mara 16 huku Leicester City wakiwa na ushindi mara 3 tu, sare baina yao ni 7.

Kwenye michezo yao mitano iliyopita, Arsenal anaongoza akiwa ameshinda mara 3 huku Leicester akishinda mara mbili. Lakini kitu kibaya kwa Arsenal ni kwamba mara ya mwisho walipokwenda King Power msimu uliopita walikutana na kipigo cha 3-0.

Fomu ya timu zote kwasasa ni kwamba Leicester City wameshinda michezo yao minne kati ya mitano iliyopita huku Arsenal wakishinda mechi moja, wakifungwa 1 na michezo mitatu imekwisha kwa sare. 

Chelsea v Crystal Palace

Hii nayo ni moja kati ya mechi kali sana za leo. Chelsea watakuwa nyumbani kuwakaribisha Crystal Palace ambaye kwa wakati mwingine unaweza kumuita kuwa ni mbabe wa vigogo.

Palace bhuwa hawana mpira wa kuvutia sana lakini mara kadhaa wamekuwa wakisumbua timu kubwa na ikiwemo msimu huu tayari washapata ushindi ndani ya Old Trafford huku pia wakilazimisha sare ya 2-2 nyumbani kwa Arsenal.

Chelsea wana rekodi nzuri kuwazidi Palace, kwenye michezo 20 iliyopita wameshinda mara 14 huku Palace wakishinda mara nne na sare ni mbili tu baina yao.

Michezo mitano iliyopita baina yao ni kwamba Chelsea wameshinda mara 3 huku Palace wakishinda mara 2.

Fomu ya Chelsea kwasasa ni nzuri sana wakiwa wameshinda mechi zao tano mfululizo. Palace wao kwenye mechi zao tano zilizopita wameshinda mara mbili, wamekwenda sare mara moja na kufungwa mara mbili.

Mechi nyingine za Leo

Burnley v West Ham

Newcastle v Bournemouth 

Southampton v Everton

Tottenham v Shefield

Imeandaliwa na Jerry Mlosa