Messi Apigilia Msumari Wa Moto, Argentina Ikiitandika Brazil 1-0

16th November 2019

RIYADH, Saudi Arabia- Mshambuliaji hatari wa Barcelona, Lionel Messi usiku wa kuamkia leo ameifunga bao timu yake ya taifa ya Argentina ambalo limeiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Brazil kwenye mechi ya kirafiki

Lionel Messi
Lionel Messi
SUMMARY

Bao pekee alilofunga Messi ilikuwa ni kwenye dakika ya 13 ambapo awali ilikuwa ni mpira wa penati ambapo alipiga na uliokolewa na kipa Allison lakini alikuwa haraka kuuwahi na akafunga kutokana na rebound.

RIYADH, Saudi Arabia -Mshambuliaji hatari wa Barcelona, Lionel Messi usiku wa kuamkia leo ameifunga bao timu yake ya taifa ya Argentina ambalo limeiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Brazil kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika nchini Saudi Arabia.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Messi tangu amalize kifungo chake cha miezi mitatu ambacho alipewa tangu mwezi Julai kwa kosa la kuiongelea mbovu michuano ya Copa America.

Bao pekee alilofunga Messi ilikuwa ni kwenye dakika ya 13 ambapo awali ilikuwa ni mpira wa penati ambapo alipiga na uliokolewa na kipa Allison lakini alikuwa haraka kuuwahi na akafunga kutokana na rebound.

Brazil ndiyo walikuwa na nafasi ya kuanza kuongoza kupitia mkwaju wa penati ambapo mshambuliaji wa Man City, Gabriel Jesus alikosa.

Kipigo hicho kinawafanya Brazil kuwa bila ya ushindi kwenye michezo mitano iliyopita tangu waliposhinda taji la Copa America.

Mechi inayofuata ya kirafiki, Argentina wanatarajia kucheza dhidi ya Uruguay kwenye mji wa Tel Aviv siku ya Jumatatu lakini mechi hiyo ina hati hati ya kughairishwa kutokana na machafuko ya nchini Isreal.

Nao Brazil watakuwa Abu Dhabi kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Korea Kusini siku ya Jumanne.

Mechi Nyingine Ya Kirafiki

Hungary 1-2 Uruguay

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya