Mechi Ya Kirafiki: Brazil Kupina Ubavu Dhidi Ya Argentina Nchini Saudi Arabia

15th November 2019

RIYADH, Saudi Arabia- Leo majira ya saa mbili usiku ndani ya uwanja wa Chuo Kikuu cha King Saud kutakuwa na pambano la kukata na shoka la kirafiki baina ya mahasimu wawili wa soka la Marekani ya Kusini, Brazil v Argentina.

Messi
Messi
SUMMARY

Kwenye mchezo wa leo kwa mara ya kwanza tunaweza kupata fursa ya kumuona mshambuliaji hatari duniani Lionel Messi akirejea kwenye kikosi chake cha Argentina baada ya miezi minne tangu alipotolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Chile kwenye michuano ya Copa America, Julai mwaka huu.

Baada ya tukio hilo, Messi alifungiwa kwa miezi mitatu baada ya kusema kuwa michuano hiyo imegubikwa na rushwa.

Kiungo wa Aston Villa, Douglas Diaz pia anaweza akaonekana kwa mara kwanza kwenye timu ya taifa akiiwakilisha Brazil.

Neymar bado atakuwa nje ya uwanja tangu alipopata tatizo la nyama za paja wakati alipokuwa akiitumikia Brazil kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria, Oktoba 13 lakini mshambuliaji wa Man City, Gabriel Jesus yupo ndani ya kikosi.

Hii ni mechi ya kwanza kwa wababe hao kukutana tangu Brazil walipopata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Copa America iliyofanyika mapema mwaka huu.

Wababe hao wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na fomu tofauti. Brazil hawajashinda kwenye michezo minne iliyopita safari ambayo ilianzatangu walipofungwa 1-0 na Peru.;

Wenzao Argentina hawajafungika kwenye michezo minne iliyopita tangu walipoanza kumkosa Messi na kwenye mechi ya mwisho waliwafunga Ecuador bao 6-1.

Katika miaka 10 iliyopita, Brazil wamekuwa ni wababe zaidi wakishinda mara 7 kati ya mechi 12 walizocheza. Mechi 2 zimekwisha kwa sare huku Argentina wao wakishinda mara 3 tu.

Baada ya mchezo huu, Argentina walikuwa wamepanga kucheza mechi nuyingine ya kirafiki dhidi ya Uruguay mjini Tel Aviv, hata hivyo mechi hiyo ina hati hati ya kutofanyika kutokana na machafuko ndani ya Israel.

Brazil wao wanajipanga kucheza na Korea Kusini, Jumanne ijayo ndani ya Abu Dhabi.

Mechi Nyingine Ya Kirafiki

Hungary v Uruguay

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya