Mbwana Samatta Azigonganisha Newcastle United Na West Ham United

8th November 2019

NEWCASTLE, Uingereza- Nyota ya nohodha wa Tanzania, Mbwana Samatta inazidi kung'aa baada ya hii leo vyombo vya habari vikubwa nchini Uingereza kusema kuwa mshambuliaji huyo anahitajika ndani ya EPL .

Mbwana Samatta
Mbwana Samatta
SUMMARY

Inaelezwa kuwa makocha wa timu hizo mbili Steve Bruce na Manuel Pellegrin wanavutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliisaidia timu yake kunyakuwa ubingwa wa ligi huku yeye akifunga mabao 25.

Kwa mujibu wa Shirikia la Utangazaji la Uingereza, BBC Sport wameripoti kuwa klabu ya Newcaste na West Ham zinapigana vikumbo kumuwania Samatta ambaye siku chache zilizopita alifunga bonge la bao ndani ya Anfield akiwa na timu yake ya Genk.

Taarifa ya BBC imekwenda mbali zaidi na kufichua kipengele cha mkataba ambacho kinamruhusu Samatta kuuzwa kwenye klabu nyingine endapo timu itakayomuhitaji itakuwa tayari kutoa paundi milioni 10.

Inaelezwa kuwa makocha wa timu hizo mbili Steve Bruce na Manuel Pellegrin wanavutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliisaidia timu yake kunyakuwa ubingwa wa ligi huku yeye akifunga mabao 25.

Hadi kufikia hapa msimu huu Samatta ameshacheza mechi 13 na amefunga mabao 6.

Samatta alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya