Mahaba Mazito: Eti Wenger Alikataa Ofa Kibao Uingereza Kwasababu Ya Mahaba Yake Kwa Arsenal

8th October 2019

LONDON, Uingereza- kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa klabu nyingi zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza zimekuwa zikihitaji huduma yake lakini anahofia sana kurudi kwasababu bado ana mapenzi na Arsenal.

Arsene Wenger
Arsene Wenger
SUMMARY

Kumekuwa na tetesi za kocha huyo kutakiwa na baadhi ya timu kubwa ikiwemo Manchester United ambayo hivi sasa imekuwa na mwendo wa kusuasua chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Alipoulizwa ni klabu zipi, babu Wenger amesema kuwa hawezi kuzitaja kwasababu itakuwa ni sawa na kuwavunjia heshima makocha waliopo kwenye klabu hizo kwa sasa.

Wenger aliondoka Arsenal kabla ya kuanza kwa msimu uliopita ikiwa ni baada ya kuifudisha klabu hiyo kwa miaka 22 ambapo alifanikiwa kumaliza ndani ya nne bora kwa miaka 20 mfululizo.

Kumekuwa na tetesi za kocha huyo kutakiwa na baadhi ya timu kubwa ikiwemo Manchester United ambayo hivi sasa imekuwa na mwendo wa kusuasua chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.

"Niliamua kutoka nje ya Uingereza kwasababu bado nina ukaribu sana na Arsenal, nimepata nafasi nyingi sana za kufanya kazi Uingereza lakini nimezipiga chini," amesema Wenger ambaye anatarajia kutimiza miaka 70 mwezi huu.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya