Ligi Kuu Bara: Simba Yabanwa Mbavu Na Tanzania Prison Nyumbani

8th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa ndani ya dimba la Uhuru, Dar es salaam ambapo tumeshuhudia Simba wakiwa nyumbani wameshindwa kutamba mbele ya Tanzania Prison

Simba vs Tanzania Prisons
Simba vs Tanzania Prisons
SUMMARY

Timu zote ziliweza kutengeneza nafasi ya kufunga ili kuibuka na ushindi lakini hakuna ambaye aliweza kutumbukiza mpira wavuni kwa dakika zote 90.

DAR ES SALAAM, Tanzania -Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa ndani ya dimba la Uhuru, Dar es salaam ambapo tumeshuhudia Simba wakiwa nyumbani wameshindwa kutamba mbele ya Tanzania Prison baada ya mchezo kumalizika kwa 0-0.

Hata hivyo sare hiyo bado imewaacha Simba kwenye nafasi yao ya kwanza kileleni wakifikisha alama 22 huku Prison wakipanda hadi nafasi ya pili baada ya kufikisha alamama 19.

Mchezo wa leo baina ya timu hizo ulitarajiwa kuwa mgumu hasa kutokana na fomu nzuri ya timu zote mbili kwasasa. Kwenye michezo mitano iliyopita kabla ya kufika leo, Simba walikuwa wamekusanya alama 12 huku Prison wakiwa wamezoa alama 9.

Timu zote ziliweza kutengeneza nafasi ya kufunga ili kuibuka na ushindi lakini hakuna ambaye aliweza kutumbukiza mpira wavuni kwa dakika zote 90.

Sare hii ina maana kuwa Prison waambulia alama ya kwanza kutoka kwa Simba baada ya kushindwa kufanya hivyo tangu mwaka 2016. Kwenye michezo mitano iliyopita timu hizo mbili zilipokutana Simba wamefunga Prison mechi zote tena hawakuruhusu bao hata moja.


Imeandaliwa na Badrudin Yahaya