Ligi Kuu Bara: Siboma, Molinga Waongeza Kilio Kwa Alliance CCM Kirumba

30th November 2019

MWANZA, Tanzania- Washambuliaji wa Yanga wa kimataifa Patrick Sibomana na David Molinga wamezidi kung'aa ndani ya kikosi hicho baada ya leo kuiwezesha timu yao kuibuka na ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Alliance.

Yanga SC
Yanga SC
SUMMARY

Dakika ya 72 ya mchezo mshambuliaji Molinga alifanikiwa kuwarejesha tena Yanga kwenye uongozi baada ya kufunga bao la pili ambalo pia ndiyo la ushindi kwenye mchezo huo.

Ushindi huo ni wa tano mfululizo kwa Yanga na watatu kwa kocha wa muda Charles Mkwasa katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu bara. 

Kwa upande wa Alliance hiki ni kipigo cha pili nyumbani baada ya kukubali kibano cha mabao 5-0 siku ya Jumanne kutoka kwa Azam.

Yanga ambao waliingia kwenye mechi hii bila ya nyota wao wa tano wa kikosi cha kwanza walianza vizuri mchezo huo kwa kushambulia mfululizo na walifanikiwa kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 25 kupitia Sibomana.

Bao hilo lilidumu hadi mapumziko ambapo Alliance hawakuonesha dalili yoyote ya kutaka kusumbua mahakama.

Hata hivyo dakika ya 10 tangu kuanza kipindi cha pili Alliance walifanikiw kuchomoa bao kupitia mshambuliaji wao Juma Nyagi.

Bao hilo lilionesha kuwainua wachezaji pamoja na mashabiki wao waliojitokeza uwanjani na walianza kucheza kwa kujiamini huku Yanga wakionekana kushikwa na bumbu wazi.

Dakika ya 72 ya mchezo mshambuliaji Molinga alifanikiwa kuwarejesha tena Yanga kwenye uongozi baada ya kufunga bao la pili ambalo pia ndiyo la ushindi kwenye mchezo huo.

Hilo linakuwa bao la nne  kwenye mechi sita kwa Mcongoman huyo ambaye amesajiliwa mwanzo wa msimu huu kuziba nafasi ya Makambo.

Kaseke, Sibomana Wazaliwa Upya

Tangu kuondoka kwa kocha Mwinyi Zahera wachezaji ambao wameonekana kuwa na athari kubwa chanya kwenye kikosi cha Yanga ni Deus Kaseke na Sibomana.

Ingawa Kaseke hajafunga hata bao moja lakini mchango wake uwanjani umekuwa mkubwa akitukumbusha kiwango chake cha zamani wakati akiwa Mbeya City.

Naye Sibomana ameonesha kuwa mchezaji hatari akifunga bao kwenye michezo yote mitatu aliyocheza chini ya Mkwasa.

Matokeo Mengine

Kagera Sugar 0-0 Ndanda

Imeandaliwa na Raheem Mohamed