Ligi Kuu Bara: Meddie Kagere, Salum Mayanga Washinda Tuzo Za Mwezi Agosti

11th September 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania -Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu bara. Kwenye mchezo huo, Kagere alifunga mabao mawili na kutengeneza lingine moja lililofungwa na Miraj Athuman. Kagere ambaye ni mfungaji bora wa msimu uliopita ameweza kuwashinda Lucas Kikoti (Namungo) na Seif Karihe kwenye kinyang'anyiro hicho. Kwa upande mwingine, kocha wa Ruvu Shooting, Salum Mayanga amefanikiwa kushinda tuzo ya kocha bora wa mwezi huo baada ya kuisadia timu yake kuibuka na ushindi wa 1-0 mbele ya Yanga kwenye mchezo uliofanyika dimba la Uhuru, Dar es salaam. Ushindi huo ulikuwa ni wa kushtukiza kwa Wapiga Kwata hao ambao walikuwa hawana rekodi ya kuwafunga Yanga tangu walipopanda daraja kwa mara ya kwanza. Hadi kufikia sasa ligi hiyo imechezwa kwa mzunguko mmoja na inataraji kuendelea tena kwa mzunguko wa pili mwishoni mwa wiki hii baada ya kuisha kwa majukumu ya timu za taifa. Imeandaliwa na Rahim Mohamed