Ligi Kuu Bara: Makame Acheka Na Nyavu Yanga Wakiitandika Coastal Union Na Kulamba Milioni 10

6th October 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania -Bao la kiungo Abdulaziz Makame dhidi ya Coastal Union, leo limeipa Yanga ushindi wa kwanza tangu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania bara

Yanga
Yanga
SUMMARY

Pamoja na ushindi huo Yanga bado imeonekana kuwa na tatizo kubwa kwenye ushambuliaji ambapo leo iliweza kutengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini ilishindwa kuzitumia ipasavyo.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi nne na kujiondoa nafasi ya 19 iliyokuwepo kabla ya mchezo wa leo.

Pamoja na ushindi huo Yanga bado imeonekana kuwa na tatizo kubwa kwenye ushambuliaji ambapo leo iliweza kutengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini ilishindwa kuzitumia ipasavyo.

Mshambuliaji David Molinga licha ya kutofunga lakini leo aliweza kuonyesha uwezo mkubwa kiasi cha mashabiki wa timu yake kumshangilia.

Coastal Union walionekana kuzidiwa tangu awali na kuwaruhusu Yanga kuumiliki mchezo huku wao wakipiga shuti moja pekee kwenye lango la Yanga ambalo pia lilipaa juu.

Kipindi cha pili Yanga walikianza kwa kasi na kulishambulia sana lango la wageni wao Coastal Union ambapo kona iliyochongwa na Mrisho Ngassa ilitua kichwani kwa Makame dakika ya 51 na kuiandikia timu yake bao hilo lililodumu hadi mwisho wa mchezo.

Baada ya bao hilo Coastal walikuja juu na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Yanga lakini ulinzi wa vijana wa kocha Mwinyi Zahera, walikwa imara na kudhibiti hatari hizo 

Beki Kelvin Yondani hakuweza kumaliza mchezo baada ya kuumia dakika ya 75 na nafasi yake kuchukuliwa na Mustapha Suleiman.

Baada ya mchezo huo kumalizika Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk. Mshindo Msolla aliwakabidhi wachezaji wa timu yake kitita cha Sh. 10 milioni kutoka kwa GSM ukiwa ni utaratibu mpya waliouanzisha endapo timu inaibuka na ushindi.

Imeandaliwa na Rahim Mohamed