La Liga: GSM Waipa Ushindi Barcelona Mbele Ya Eibar

19th October 2019

BARCELONA, Hispania- Washambuliaji wapya wa Barcelona, Antoine Griezmann, Luis Suaraz na Lionel Messi kila mmoja amefunga bao moja na kuiwzesha timu yao kuibuka na ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Eibar kwenye mchezo wa La Liga.

Lionel Messi
Lionel Messi
SUMMARY

Ushindi huu umekuja siku moja mara baada ya La Liga kutangaza kufuta mchezo wa El Classico uliopangwa kuchezwa Now Camp wiki ijayo. 

Huu ni ushindi wa tano mfululizo kwa timu hiyo kwenye michuano yote na umewapeleka kileleni kwa muda kabla ya Real Madrid kushuka dimbani kwenye mchezo wao wa usiku dhidi ya Mallorca.

Barcelona wangeweza kufunga mabao mengi zaidi kama si kipa Marko Dmitrovic wa wenyeji Eibar kuwa makini langoni.

Suarez aliweza kufunga bao lingine ambalo lilikataliwa kwa madai ya kuwa alikuwa ameotea.

Ushindi huu umekuja siku moja mara baada ya La Liga kutangaza kufuta mchezo wa El Classico uliopangwa kuchezwa Now Camp wiki ijayo. 

Kumekuwa na siku kadhaa za vurugu ndani ya mji wa Cataluna tangu baadhi ya viongozi wa wanaharakati kufungwa jela siku ya Jumatatu.

Iliwabidi Barcelona kuondoka mapema tangu siku ya Alhamisi ili tu wasishindwe kusafiri kwa wakati kutokana na machafuko.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya