Kwaheri Ya Kuonana: David Villa Atangaza Kutindika Daluga Baada Ya Miaka 19

13th November 2019

TOKYO, Japan -Mfungaji bora wa timu ya taifa ya Hispania, DaviD Villa ametangaza nia yake ya kustaafu soka la ushindani mapema mwezi ujao wakati ligi kuu ya Japan itakapofika mwisho.

David Villa
David Villa
SUMMARY

"Nimelifikiria jambo hili kwa muda mrefu uliopita, nimeamua kustaafu mpira na wala sijalazimishwa kustaafu," amesema kwenye taarifa yake.

TOKYO, JapanĀ -Mfungaji bora wa timu ya taifa ya Hispania, DaviD Villa ametangaza nia yake ya kustaafu soka la ushindani mapema mwezi ujao wakati ligi kuu ya Japan itakapofika mwisho.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona anatarajia kumaliza maisha yake ya soka baada ya miaka 19 huku akiwa ameshinda kombe la dunia 2010 pamoja na lile la Euro 2008 akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania.

Villa, 37 pia ameshinda mataji ya La Liga pamoja na ligi ya mabingwa ulaya akiwa na timu ya FC Barlecona.

"Nimelifikira jambo hili kwa muda mrefu uliopita, nimeamua kustaafu mpira na wala sijalazimishwa kustaafu," amesema kwenye taarifa yake.

Villa kwasasa anacheza timu ya Vissel Kobe inayoshiriki ligi ya nchini Japan na alijiunga na timu hiyo tangu mwanzo wa msimu akitokea Marekani ambapo alicheza kwenye timu ya New York City kwa misimu minne mfululizo.

Mshambuliaji huyo amefunga mabao 59 kwa timu ya taifa ya Hispania akicheza kwenye michuano mitatu ya kombe la dunia na kushinda taji mara moja mwaka 2010 ikiwa ni miaka miwili baada ya kushinda taji la Euro mwaka 2008.

Villa anakumbukwa kwa kufunga bao safi dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya uliofanyika Wembley msimu wa 2010-11 ambapo Barcelona walishinda 3-1.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya