Kuzufu Euro 2020: Cristiano Ronaldo Kuandika Rekodi Hii Ya Dunia Leo Dhidi Ya Ukraine?

14th October 2019

KYIV, Ukraine- Cristiano Ronaldo leo usiku anashuka dimbani kuwaongoza timu ya taifa ya Ureno kwenye mchezo muhimu wa kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Euro 2020.

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo
SUMMARY

Hata kama leo Ronaldo atashindwa kufanya hivyo basi atajaribu bahati hiyo wikiendi ijayo akirudi Juventus wakati timu yake itakapokuwa ikicheza dhidi ya Bologna kwenye mchezo wa Serie A kwani takwimu hizi zinajumlisha mabao ya klabu na timu ya taifa.

Mbali na umuhimu wa mchezo huo kwa pande zote mbili lakini pia staa huyo wa Juventus, Ronaldo atakuwa na nafasi ya kuingia kwenye rekodi nyingi kali za kusisimua duniani kwenye upade wa upachikaji wa mabao.

Hadi sasa Ronaldo amefunga mabao 699 kwenye mechi za ushindani tangu alipoanza soka na endapo atafunga leo atafanikiwa kuingia kwenye rekodi ya wanaume watano ambao wao wapo kwenye idadi ya mabao 700 na kuendelea.

Hata kama leo Ronaldo atashindwa kufanya hivyo basi atajaribu bahati hiyo wikiendi ijayo akirudi Juventus wakati timu yake itakapokuwa ikicheza dhidi ya Bologna kwenye mchezo wa Serie A kwani takwimu hizi zinajumlisha mabao ya klabu na timu ya taifa.

Je ni wachezaji gani ambao wapo juu ya mabao 700 hadi hivi sasa ambao Ronaldo anatakiwa kufika kwenye anga zao? SportPesa News inakusogezea vipanga hao kiganjani mwako.

Josef Bican (Mabao 805)

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Czechoslovakia na klabu za Slavia Prague na Radip Vienna.

Inakadiriwa kuwa amefunga mabao 805 katika mechi zote za kimashindano kwa klabu na timu ya taifa. Kati ya mabao hayo, 600 ni kwenye michezo ya ligi tu.

Alizaliwa mwaka 1913 na alifariki mwaka 2001 akiwa na miaka 88. Alianza kucheza soka mwaka 1928 na alistaafu mwaka 1955 ambapo aligeukia ukocha na kufundisha timu mbalimbali hadi mwaka 1977 alipostaafu.

Romario (Mabao 734)

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu kadhaa barani Amerika na ulaya. 

Amewahi kucheza kwenye timu za Barcelona, PSV wakati akiwa Ulaya lakini amecheza kwenye timu za Flamengo, Vasco da Gama, Fluminense akiwa nchini kwao Brazil.

Katika klabu zote hizo ambazo amewahi kucheza, Romario amefunga jumla ya mabao 679 na pia amefunga mabao 55 akiwa na timu yake ya taifa na kumfanya kufikisha idadi ya mabao 734 kwenye maisha yake ya soka tangu alipoanza kucheza mwaka 1985 hadi alipostaafu mwaka 2009.

Pele (Mabao 722)

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu za Santos na New York Cosmos. Wengi wanasema kuwa ni mfalme wa soka hadi hivi sasa ingawa vijana wengi wa zama hizi hawajapata kumuona akicheza.

Kumekuwa na dhana nyingi kuhusu idadi yake ya mabao aliyofunga wakati akicheza soka na kwa upande wetu tumechukuwa idadi ambayo imetajwa kuwa ni ile rasmi kwenye mechi za ushindani tu.

katika maisha yake ya soka Pele amecheza kwenye klabu mbili tofauti ambazo ni Santos na hapo alifunga mabao 619 kwenye mechi 638 alizocheza tangu 1956 hadi 1974.

Alivvyotoka hapo alihamia kwenye timu ya New York Cosmos ambapo alicheza kwa miaka miwili tangu mwaka 1975 hadi 1977 na alifanikiwa kucheza mechi 56 na kufunga mabao 31.

Kwa ujumla kwenye klabu hizo mbili alifunga jumla ya mabao 650. Akiwa na timu ya taifa amecheza michezo 92 na amefunga mabao 77.

Kwa maana hiyo Pele amefunga mabao 722 kwenye maisha yake ya soka wakati wa mechi za ushindani tangu alipoanza kucheza mwaka1956 hadi alipostaafu mwaka 1977.

Gerd Muller (Mabao 721)

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich. Amefunga mabao 653 akiwa na timu za klabu kwenye mechi za mashindano.

Kwenye upande wa timu ya taifa amefunga mabao 68 akiwa ni miongoni mwa wafungaji bora ambao wameingia kwenye orodha hiyo akiwa amecheza mechi chache kuliko wote (mechi 62).

Idadi ya mabao 653 kwenye klabu na 68 timu ya taifa ndiyo inayomfanya kuwa na jumla ya mabao 721 kwenye maisha yake ya soka tangu alipoanza kucheza mwaka 1963 hadi alipostaafu mwaka 1981.

Ferenc Puskas (Mabao 706)

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Hungary na Hispania, alicheza pia kwenye timu ya Real Madrid.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo ni kwamba Puskas amefunga mabao 622 kwenye ngazi ya timu za klabu laki pia amefunga mabao 84 kwenye timu ya taifa.

Idadi hiyo ya mabao inamfanya kufikisha jumla ya mabao 706 aliyofunga kwenye maisha yake ya soka tangu alipoanza kucheza mwaka 1943 hadi alipostaafu mwaka 1966.

Huyu alikuwa naye ni kipanga hasa wa kupachika mabao na hadi kufikia tuzo ya goli bora la dunia ikapewa jina lake "Puskas Award".

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya