Kombe La Dunia Rugby: Japan Yapania Kutinga Nusu Fainali Kupitia Mgongo Wa Afrika Kusini

19th October 2019

TOKYO, Japan- Mchezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa Rugby ya Japan, Lappies Labuschagne amesema kuwa yeye pamoja na wachezaji wenzake wamepania kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia

Japan
Japan
SUMMARY

Japan walifanikiwa kuwafunga wababe Afrika Kusini mara ya mwisho walipokutana kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la dunia mwaka 2015.

TOKYO, Japan -Mchezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa Rugby ya Japan, Lappies Labuschagne amesema kuwa yeye pamoja na wachezaji wenzake wamepania kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa kuwaondosha Afrika Kusini kwenye mchezo wao wa Jumapili.

Japan ambao ni wenyeji wa michuano hiyo watavaana na Afrika Kusini kwenye mchezo wa robo fainali uliopangwa kufanyika kwenye dimba la Tokyo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Labuschagne ambaye ni mzaliwa wa Afrika Kusini amesema kuwa tumejipanga kukabiliana na kila timu itakayokuja mbele yetu na mwisho kushinda taji.

"Kiukweli tumepijapanga kukabiliana na timu zote zinazokuja mbele yetu, hatujapanga kuishia kwenye hatua ya robo fainali," amesema.

Labuschagne, 30, amesema kuwa ingawa yeye ni mzaliwa wa Afrika Kusini lakini kwasasa yeye ni raia wa Japan na hivyo atapambana kwa ajili ya kulitetea taifa lake mwanza hadi mwisho.

Japan walifanikiwa kuwafunga wababe Afrika Kusini mara ya mwisho walipokutana kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la dunia mwaka 2015.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya