Kikapu: Kyle Lowry Kusaini Mkataba Mpya Toronto Raptors Wenye Thamani Ya Bilioni 71.2 Kwa Mwaka

8th October 2019

TORONTO, Marekani- Mabingwa watetezi wa ligi ya kikapu ya Marekani maarufu NBA, Toronto Raptors wameanza mpango wa kukisuka kikosi chao

Kyle Lowry
Kyle Lowry
SUMMARY

Lowry ambaye kikawaida huwa anacheza kwenye nafasi ya ulinzi alisaini mkataba wa miaka mitatu na Raptors mnamo mwaka 2017 uliokuwa na thamani ya dola milioni 100. 

TORONTO, Marekani- Mabingwa watetezi wa ligi ya kikapu ya Marekani maarufu NBA, Toronto Raptors wameanza mpango wa kukisuka kikosi chao huku wakikabiliana dili la dola milioni 31 (zaidi ya shilingi bilioni 71) ili kumuongezea mkataba mchezaji wao wa nafasi ya ulinzi, Kyle Lowry.

Hela hiyo ni majumuisho ya mshahara pamoja na posho zake kama mchezaji ndani ya msimu mzima wa NBA ambao unatarajiwa kuanza Oktoba 22, mwaka huu.

Lowry alikuwa anaelekea kumaliza mkataba na timu hiyo na tayari timu kadhaa kubwa zinazoshiriki ligi hiyo zilikuwa zinamnyatia kwa ajili ya kumpa mkataba kutokana na kiwango bora alichoonesha msimu uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na ESPN ni kwamba Lowry amekubaliana dili hilo na timu yake ya Raptors na sasa anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka klabuni hapo hadi mwaka 2021.

Lowry ambaye kikawaida huwa anacheza kwenye nafasi ya ulinzi alisaini mkataba wa miaka mitatu na Raptors mnamo mwaka 2017 uliokuwa na thamani ya dola milioni 100. 

Kwa mara ya kwanza Lowry alijiunga na Raptors mwaka 2012 akiisaidia timu hiyo kurudi kwenye ushindani na hadi kufikia kushinda taji msimu uliopita.

Lowry amekuwa kwenye kiwango bora ndani ya ligi ya NBA kitu kilichofanya amechaguliwa mara tano mfululizo kwenye kikosi cha All Stars.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya