Kikapu: Jeraha La Mkono Kumuweka Stephen Curry Nje Kwa Miezi Mitatu

2nd November 2019

CALIFORNIA, Marekani- Majangaa! Habari mbaya kwa mashabiki wa timu ya mpira wa kikapu ya Golden State Warriors ni kwamba staa wao Stephen Curry atakuwa nje ya uwanja wa takribani miezi mitatu au zaidi

Stephen Curry
Stephen Curry
SUMMARY

Curry alivunjika mkono wa kushoto katikati ya wiki hii wakati timu yake ikipokea kichapo kutoka kwa Phoenix Suns na sasa ataiacha timu hiyo kwenye wakati mgumu zaidi.

CALIFORNIA, Marekani -Majangaa! Habari mbaya kwa mashabiki wa timu ya mpira wa kikapu ya Golden State Warriors ni kwamba staa wao Stephen Curry atakuwa nje ya uwanja wa takribani miezi mitatu au zaidi baada ya kufanyiwa operesheni ya mkono

Curry alivunjika mkono wa kushoto katikati ya wiki hii wakati timu yake ikipokea kichapo kutoka kwa Phoenix Suns na sasa ataiacha timu hiyo kwenye wakati mgumu zaidi.

Timu hiyo imeanza msimu vibaya kwa kufungwa michezo mitatu kati ya minne walioshuka dimbani msimu huu.

Kuondoka kwa Kevin Durant aliyetimkia Brooklyn Nets mwisho wa msimu uliopita na kuumia kwa Klay Thompson kuliiyumbisha Warriors ambapo staa aliyebaki akitegemewa alikuwa ni Curry peke yake amabaye naye sasa ameumia.

Kwa mujibu wa ratiba ya NBA, Curry anatarajia kurudi uwanjani kipindi ambacho kutakuwa na mechi za All Stars huko Chicago.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya