Kikapu: James Harden, Russell Westbrook Wathibitisha Kushiriki Olimpiki Tokyo 2020

9th October 2019

SAN FRANCISCO, Marekani- Wachezaji wa timu ya Houston Rockets inayoshiriki ligi ya NBA, James Harden na Russell Westbrook wamesema kuwa wataiwakilisha nchi ya Marekani kwenye michuano ya Olimpiki

James Haden
James Haden
SUMMARY

Timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Marekani imeshiriki michuano ya kombe la dunia mpira wa kikapu (FIBA) nchini China mwezi uliopita lakini walifanya vibaya mno baada ya kumaliza kwenye nafasi ya saba kitu ambacho hakijawahi kutokea hapo awali.


SAN FRANCISCO, Marekani -Wachezaji wa timu ya Houston Rockets inayoshiriki ligi ya NBA, James Harden na Russell Westbrook wamesema kuwa wataiwakilisha nchi ya Marekani kwenye michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika Tokyo, Japan mwaka 2020.

Nyota hao wataungana na Stephen Curry na Damian Lillard wa timu ya Golden State Warriors pamoja na Anthony Davis wa Los Angeles Lakers ambao wao tayari pia wamethibitisha kuwa watakuwa tayari kushiriki kwenye michuano hiyo ya Olimpiki.

Timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Marekani imeshiriki michuano ya kombe la dunia mpira wa kikapu (FIBA) nchini China mwezi uliopita lakini walifanya vibaya mno baada ya kumaliza kwenye nafasi ya saba kitu ambacho hakijawahi kutokea hapo awali.

Katika mashindano hayo, nyota wengi raia wa Marekani wanaocheza ligi ya mpira wa kikapu ya NBA hawakushiriki kwasababu zao mbalimbali na kufanya timu hiyo kwenda na kikosi cha kawaida ambapo Spain walifanikiwa kushinda taji baada ya kuwafunga Argentina kwenye mchezo wa fainali.

"Itakuwa ni heshima kubwa kwangu kama nitaitwa kwenda kuiwakilisha nchi yangu Tokyo, Japan, nitapenda zaidi kucheza na kujitolea," amesema Harden baada ya kuulizwa kama atapenda kwenda na timu ya taifa nchini Japan kwenye michuano ya Olimpik.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya