Kikapu: JKT Yaanza Vyema Michuano Ya Klabu Bingwa Afrika

17th October 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Timu ya JKT Wanaume imeanza vyema mashindano ya klabu bingwa Afrika ya mchezo wa Basketball baada ya kuifunga timu ya Hawasa City ya Ethiopia kwa pointi 87 kwa 47.

Basketball ball
Basketball ball
SUMMARY

Mashindano hayo yameanza jana jioni na yatafanyika kwa siku nne hadi tarehe 20, na washindi wawili kutoka katika kila kundi watacheza hatua ya mtoano kutafuta wawakilishi wa ligi ya mabingwa ya mchezo wa Basketball Afrika.

Katika mchezo huo wa ufunguzi wa kundi D uliofanyika uwanja wa ndani wa taifa (In door), ilimshuhudia mchezaji Ramadhani Said, akifunga pointi 23 na kuisaidia timu yake kuanza vizuri mashindano hayo makubwa Afrika.

Hawasa City ilijaribu kupambana katika robo ya kwanza baada ya kufunga pointi sita za haraka lakini wawakilishi wa Tanzania JKT walitulia na kujipanga vyema hadi kuibuka na ushindi.

Mashindano hayo yameanza jana jioni na yatafanyika kwa siku nne hadi tarehe 20, na washindi wawili kutoka katika kila kundi watacheza hatua ya mtoano kutafuta wawakilishi wa ligi ya mabingwa ya mchezo wa Basketball Afrika.

Imeandaliwa na Rahim Mohamed