Kikapu: Haya Ndiyo Makubwa 5 Yaliyojiri Tangu Kuanza Kwa Ligi Ya NBA Wiki Iliyopita

30th October 2019

TORONTO, Marekani- Siku saba zimekatika tangu ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani ilipoanza Jumanne iliyopita.

NBA
NBA
SUMMARY

Baada ya kutawaliwa na majirani zao LA Lakers kwa misimu mingi, hatimaye LA Clippers nao wamepata timu ya ushindani.

Tayari miamba imeshaanza kutambiana kwa kuoneshana ubabe na kama kawaida SportPesa News tukayadaka makumbwa 5 yaliyojiri ndani ya wiki moja hiyo.

Kyrie Irving Afanya Balaa

Ndani ya wiki moja hii, kijana Kyrie Irving amefanya mambo makubwa ambayo hakuna mwingine aliyeyakaribia hata kidogo.

Kwnye mchezo wake wa kwanza tu akiwa na timu yake mpya ya Brooklyn Nets, Irving alifunga jumla ya vikapu 50 kitu ambacho siyo kawaida kutokea.

Alikwenda mbali zaidi baada ya kufunga vikapu 26 kwenye mechi ya pili na vikapu 37 kwenye mechi ya tatu na kumfanya kuwa amefunga vikapu 113 ndani ya wiki ya kwanza ya NBA.

Zama Za GSW Zimefika Mwisho

Zama za utawala wa miaka mitano wa Golden State Warriors na Stephen Curry zinaonekana kuelekea ukingoni.

Hii ni baada ya kuanza vibaya msimu huu wakifungwa mechi zote mbili za awali kitu ambacho hakijawahi kuwatokea kwa miaka zaidi ya kumi iliyopitaa. 

Hata hivyo jana waliweza kupata ushindi wao wa kwanza wa msimu dhidi ya vibonde New Orleans Pelicans.

Lakini tatizo lao litakalo wasumbua msimu huu nadhani bado lipo, walishindwa kumsajili mbadala wa Kevin Durant aliyeondoka baada ya msimu uliopita kuisha lakini pia wanahangaika kupata mbadala wa Klay Thomspon ambaye ni majeruhi na atakuwa nje kwa takribani msimu mzima.

LA Clippers Hawapoi Hawaboi

Baada ya kutawaliwa na majirani zao LA Lakers kwa misimu mingi, hatimaye LA Clippers nao wamepata timu ya ushindani.

Wamewafunga Lakers kwenye mechi ya kwanza tu ya msimu na tangu ambapo wameshinda mechi nyingine mbili huku wakifungwa mara moja katika mechi nne walizoshuka dimbani msimu huu.

Kawhi Leonard kama alivyofanya msimu uliopitya akiwa na Toronto Raptors anaendelea pale alipoishia na safari hii anafanya kazi nzuri ndani ya Clippers timu ambayo imetabiriwa kufanya vizuri msimu huu.

Brooklyn Nest Wazee Wa OT

Hii sijui tuiite ni bahata mbaya au uzembe mimi sijui bhana! lakini Brooklyn wamekuwa timu inayoongoza kufungwa kwenye Over Time (OT).

Licha ya kuwa na nyota anayefunga vikapu vingi Kyrie Irving lakini kwenye michezo mitatu ya awali wamefungwa mara mbili kwenye OT na wao wameshinda mchezo mmoja tu.

Kwenye mechi dhidi ya Memphis walifungwa kwenye OT kwa jumla ya vikapu 134-133 na kwenye mechi dhidi ya Minnesota pia walifungwa kwa vikapu 126-126 kwa mtindo huo huo wa OT.

Mechi pekee waliyoibuka na ushindi ni dhidi ya New York Knicks ambapo walishinda kwa vikapu 113-109.

Kumbuka timu hii ndiyo yupo mtaalamu Kevin Durant aliyojiunga nayo msimu huu akitokea Golden State Warriors.

Philadelphia 76ers Hawafungiki

Timu ya Philadelphia ndiyo timu ambayo bado haijaonja ladha ya kipigo tangu msimu ulipoanza.

Wameshuka dimbani mara tatu na wameshinda mechi zote ambazo ni dhidi ya Boston Celtics, Detroit Pistons na Atalanta Hawks.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya