Kaanza Kuogopa?: Kisa Kuzidiwa Uzito, Mfilipino Atishia Kugoma Kuzichapa Na Mwakinyo

28th November 2019

DAR ES SALALAAM, Tanzania- Ikiwa zimebaki saa chache kabla ya pambano, bondia raia wa Philipino, Arnel Tinampay ametishia kugoma kupanda ulingo kama endapo mpinzani wake Hassan Mwakinyo hatopunguza uzito ambao umezidi mwilini kwake.

Hassan Mwakinyo
Hassan Mwakinyo
SUMMARY

"Kwenye mapambano ya ngumu watu huwa wanazidiana kwa kilo nyingi kuliko hizi na wanapigana vizuri tu, yeye kuzidiwa pointi anaona ni sababu, ila dawa yake ipo jikoni na kesho atakiona cha moto," amesema Mwakinyo ambaye ni balozi wa kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Hayo ameyasema leo mchana wakati wa shughuli ya kupima uzito na afya iliyofanyika mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es saalam.

Mwakingo amekutwa na kilogram 70 wakati Tinampay amekutwa na kiligram 69.7 na hivyo jamaa analilia hizo point kadhaa alizozidiwa zipungue kabla ya kesho ili yeye akubali kupanda ulingoni.

'Mimi sitapanda ulingoni kama huo uzito uliozidi hautapungua, haya yalikuwa ni makubaliano yetu kabla ya kusaini mkataba na ni sheria duniani kote ambayo mimi sipo tayari kwenda kinyume nayo," amesema Tinampay.

Kwa upande wake Mwakinyo amesema kuwa uzito uliozidi ni wa kawaida sana na hii ni kutokana na yeye kula chakula kwa siku ya leo. Hata hivyo amewatoa hofu Watanzania kwa kuwaambia kuwa uzito huo utapungua na pambano litafanyika kama kawaida.


"Unajua huyu jamaa ameshaanza kuniogopa na hapa anatafuta sababu ndogo ndogo, uzito uliozidi ni wakawaida na unapungua ndani ya muda mfupi tu"

"Kwenye mapambano ya ngumu watu huwa wanazidiana kwa kilo nyingi kuliko hizi na wanapigana vizuri tu, yeye kuzidiwa pointi anaona ni sababu, ila dawa yake ipo jikoni na kesho atakiona cha moto," amesema Mwakinyo ambaye ni balozi wa kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni siku ya kesho (Ijumaa) kwenye pambano la raundi 10 uzito wa kati ambalo sio la ubingwa.

Pambano hilo litafanyika ndani ya uwanja wa uhuru kwa mara ya kwanza kwenye historia ya mchezo wa ngumi nchini na tayari kumetangazwa kuwa hakutakuwa na kiingilio.

Takwimu Za Mabondia

Tinampey mwenye umri wa miaka 35 ni mzoefu zaidi ya Mwakinyo mwenye umri wa miaka 24 hado hivi sasa.

Tofauti na Mwakinyo ambaye ameingia kwenye masumbwi ya kulipwa huu ukiwa ni mwaka wake wa 4, Tinampay ana miaka 16 kwenye ulingo wa ngumi za kulipwa.


Tangu alipoanza mapambano ya kulipwa miaka 16 iliyopita jamaa amepigana mapambano 40 akishinda 21 akipigwa mara 18 na kutoka droo mara 1.

Mwakinyo kwa upande waka amepigana mara 17 ndani ya miaka minne akishinda mara 15 na kuipigwa mara mbili, hajawahi kwenda sare.

Imeandaliwa na Raheem Mohamed