Hizi Ndizo Mechi Kali Tano Hutakiwi Kuzikosa Wikiendi Hii

8th November 2019

MUNICH, Ujerumani -Ligi kuu kwenye nchi mbalimbali duniani zitashika kasi mwisho wa wiki hii. Barani Ulaya kuna zile ligi tano bora ambapo kwa uchache SportPesa News inakuletea kiganjani kwako mechi ambazo hautakiwa kuzikosa.

Roberto Lewandowski
Roberto Lewandowski
SUMMARY

Upo tayari kushinda MAMILIONI leo?

Usiishie tu kusubiria matokeo ya mechi! Bet mechi kali za leo kupitia SportPesa ujishindie MAMILIONI kwa JERO au zaidi.

Bofya HAPA kubet sasa.

MUNICH, Ujerumani -Ligi kuu kwenye nchi mbalimbali duniani zitashika kasi mwisho wa wiki hii. Barani Ulaya kuna zile ligi tano bora ambapo kwa uchache SportPesa News inakuletea kiganjani kwako mechi ambazo hautakiwa kuzikosa.

Kumbuka kuwa wiki hii ni ya mwisho kwenye ligi zote duniani na baada ya hapo kalenda ya FIFA kwa mechi za timu za taifa itafuata, hivyo ukipitwa na uhondo huu basi kuupata tena ni baada ya wiki mbili.

Bayern Munich v Borrusia Dortmud

Siku ya Jumamosi pale Allianz Arena kuna kipute cha kufa mtu ambapo Bayern Munich wenyeji watawakaribisha Borrusia Dortmund.

Uzuri wa mechi hii unatokana na ubora wa timu zote mbili kwasasa. Bayern Munich wameyumba kwa kiasi fulani na mechi yao ya mwisho ya ligi wiki iliyopita wlifungwa 5-1 na Frankfurt kitu kilochosababisha kocha Niko Kovac kutimuliwa kazi.

Wanakutana na Dortmund ambao wana moto mkubwa wakiwa nafasi ya pili kileleni. Hata hivyo licha ya Munich kuwa kwenye nafasi ya nne lakini tofauti yake na Dortmund ni alama moja tu na hivyo mchezo huo utakuwa ni wakibabe zaidi.

Liverpool v Man City

Wababe wa EPL kwasasa. Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye dimba la Anfield siku ya Jumapili huku tofauti ya alama baina yao ikiwa ni 6. Liverpool wapo juu na Man City wapo nafasi ya pili.

Mchezo wa kesho kwa kiasi fulani utatoa taswira kuelekea mbio za ubingwa. Kama Liverpool watashinda na kuongeza pointi kufikia 9 dhidi ya mpinzani wake basi ni wazi kabisa watakuwa wanajitengenezea mazingira mazuri zaidi ya ubingwa msimu huu.

Na Kama ikitokea wakafungwa na pointi kupungua hadi kufikia tatu ni wazi kabisa watakuwa wameacha wazi mbio za ubingwa kwa timu yeyote kuchukuwa.

Leicester City v Arsenal

Arsenal hawajashinda kwenye michezo miwili iliyopiota ya ligi ambayo wamecheza kwenye uwanja wa nyumbani kwao. Wanakwenda kucheza ugenini dhidi ya Leicester City ambao wapo kwenye kiwango bora sana.

Wameshinda michezo yao minne iliyopita ukiwemo ushindi wa 9-0 dhidi ya Southampton wiki mbili zilizopita.

Ama hakika mchezo huo utakuwa ni mgumu zaidi kwa Arsenal na mazingira yatakuwa mabaya zaidi kwa kocha Unai Emery ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki ambao hawaridhishwi na kile ambacho wanakiona uwanjani.

Juventus v AC Milan

Ingawa AC Milan wamepotea kwenye anga la soka la Italia lakini bado wanapokutana na vigogo wa ligi hiyo moto huwa unawaka kweli kweli.

Mchezo wao wa Jumapili hii watavaana na vinara wa ligi ya Italia, Juventus ambao wana hamu kubwa ya kupata matokeo ya ushindi ili kujikita kileleni kwakuwa wanakimbizwa kwa karibu sana na Inter Milan.

Marseille v Lyon

Siku ya Jumapili pale kwenye uwanja wa Orange Velodrome kutakuwa mechi ya kukata na shoka kwenye Ligue 1, ambapo Merseille watawakaribisha Lyon.

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa ligi ya Ufaransa utakubaliana na mimi kuwa timu hizo zina historia kubwa ndani ya nchi hiyo zikiwa zimezalisha wachezaji wengi sana ambao wametamba duniani.

Mchezo wa Jumapili utawakutanisha wakiwa na fomu tofauti, Marseille wapo kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa na alama 19 wakati Lyon wapo nafasi ya 10 wakiwa na alama 16 huku timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 12.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya