Gofu: Tiger Woods Alenga Kushiriki Michuano Ya Olimpiki Tokyo 2020

18th October 2019

CHICAGO, Marekani- Mchezaji wa gofu nguli duniani Tiger Woods amesema kuwa analenga kushiriki michuano ya olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020 ili kujiongezea moja ya rekodi ambayo haipo kwenye maisha yake.

Tiger Woods
Tiger Woods
SUMMARY

Woods ambaye alikuwa ni kama mtawala wa mchezo huo kwa kipindi cha takribani muongo sasa amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya majeruhi pamoja na masuala ya kifamilia yaliyomfanya kupoteza ubora wake aliokuwa nao hapo awali.

Mchezo wa gofu ulikuwa haupo kwenye mashindano ya olimpiki kwa kipindi cha miaka 112 na kwa mara ya kwanza ulirudishwa mwaka 2016 lakini Woods alikosekana kutoka na majeraha.

Woods ambaye alikuwa ni kama mtawala wa mchezo huo kwa kipindi cha takribani muongo sasa amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya majeruhi pamoja na masuala ya kifamilia yaliyomfanya kupoteza ubora wake aliokuwa nao hapo awali.

"Kuwemo ndani ya timu ya olimpiki ni lengo langu kubwa, sijioni kama nitakuwa na nafasi nyingine nyingi zaidi ya hii ya mwakani"

"Nikikosa safari hii basi kwenye olimpiki ijayo nitakuwa nina umri wa miaka 48 kitu ambacho kitu sio kizuri," amesema Woods.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya