Formula One: "Tulistahili Kufanya Vizuri" Perez Afunguka Baada Ta Mbio Za British GP

15th July 2019

NORTHAMPTONSHIRE, England – Dereva wa timu ya SportPesa Racing Point, Sergio Perez amesema timu yake hiyo ilistahili kufanya vizuri zaidi kwenye mbio za jana za British GP. Katika mbio hizo za jana, Perez alimaliza katika nafasi ya 17, dereva mwenzake wa SportPesa Racing Point akimaliza katika nafasi ya 13 huku dereva wa Marcedez, Lewis Hamilton akimaliza katika nafasi ya kwanza. “Siamini bahati mbaya iliyotukumba. Kiukweli inaumiza kwa sababu tulistahili kufanya vizuri katika mbio hizi. "Hatukuwa na nafasi nzuri leo. Raundi ya kwanza ilikuwa mzuri sana, nilikuwa kwenye nafasi nzuri. “Baada ya hapo gari la usalama lilipotoka tu ndiyo liliharibika mbio yangu. “Wakati huo, pia usukani wangu ulikuwa na shida na kuharibu mfumo wa breki. Ndiyo maana nikamgonga Hulkenberg kwa sababu sikuwa na uwezo wa kusimamisha gari. Nikaharibu mipango yangu na kushuka chini kabisa, " alifafanua Perez raia wa Mexico. Tusahau kilichotokea Naye dereva Lance Stroll raia wa Canada, amesema hawana budi kusahau kilichotokea hapo jana huku akidai kwamba matairi yalikwamisha malengo yake. “Tusahau kilichotokea. Nilikuwa na mwanzo mzuri ambapo nilikuwa wa tatu katika mzunguko wa kwanza. “Kwa bahati mbaya mikakati yetu haikwenda vizuri kama tulivyopanga kwani mapema tulipaswa kuondoa uchafu uliokuwa katika breki ya upande wa kushoto. “Nilisimamishwa mara mbili kwa sababu ya kubadilisha tairi. Nadhani timu yangu ilifikiri matairi ya magari yaliyotutangulia yangeshindwa kumaliza mbio lakini kwa bahati mbaya haikutokea hivyo.