Formula 2: Dereva Anthoine Hubert Azikwa Nchini Ufaransa

11th September 2019

CHARTERS, Ufaransa -Mazishi ya aliyekuwa dereva wa Formula 2, Anthoine Hubert yamefanyika na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiongozwa na wanafamilia. Hubert, 22, alifariki mwezi uliopita kwenye ajali iliyohusisha magari matatu wakati wa mashindo ya Belgium Grand Prix. Baadhi ya watu waliohudhuria ni pamoja na rafiki yake mkubwa na bingwa wa michuano ya Belgium GP na Italian GP, Charles Leclerc. Wengine ni Pierre Gasky, Esteban Ocon na George Russell. "Athoine, tabasamu lako, nguvu yako muonekano wako ndiyo vitu pekee ambavyo umetuachia," amesema Alain Prost ambaye ni bingwa wa zamani wa Formula 1 na amezungumza akiwakilisha timu ya Renault Sport Racing ambayo ilikuwa ikimmiliki Hubert. Ibada ya mazishi imedumu kwa zaidi ya saa tatu na ilikuwa ikiruka mubashara kwenye skrini kubwa nje ya kanisa. Imeandaliwa na Badrudin Yahaya