Formula 1: Valtteri Bottas Ashinda Japan GP Na Kuifanya Mercedes Kuweka Rekodi Ya Dunia

13th October 2019

TOKYO, Japan- Dereva wa Mercedes, Valterri Bottas ameshinda mbio za Japan GP na kuiweezesha kampuni yake kuweka rekodi mpya ndani ya Formula 1 ya ushindi mara mbili ndani ya msimu mmoja kwa miaka sita mfululizo.

Japan GP
Japan GP
SUMMARY

Kwenye Japan GP, mbali na Bottas aliyeshika nafasi ya kwanza, dereva wa Ferrari. Sebastian Vettel alishika nafasi ya pili mbele ya Hamilton aliyekamata nafasi ya tatu.

Ushindi wa Bottas umewahakikishia taji la msimu Mercedes licha ya kuwa bado kuna mbio nne zimebaki kabla ya msimu kuisha.

Mbali na taji hilo kwa Mercedes lakini pia dereva mwingine wa kampuni hiyo, Lewis Hamilton ana uhakika wa kushinda taji binafsi la ubingwa wa dunia na hadi kufikia sasa hakuna mwingine atakayeweza kumzuia zaidi ya dereva mwenzie ambaye ni Bottas.

Ushindi huu umevunja rekodi za ushindi mara mbili wa msimu ndani ya misimu mitano mfululizo zilizowekwa na Michael Schumacher akiwa na Ferrari kuanzia mwaka 2000-2004 na hii sasa inadhihirisha kuwa Mercedes sasa ndiyo wababe wa Formula 1.

"Kitu kama hiki hakijawahi kufanyika hapo kabla na ndiyo maana inafurahisha sana, ni Formula 1 na hii ni historia, kuna vitu vingi vya muhimu lakini kwa upande wetu hii ni nzuri sana,' amesema Boss wa Merceds, Toto Wolff.

Kwenye Japan GP, mbali na Bottas aliyeshika nafasi ya kwanza, dereva wa Ferrari. Sebastian Vettel alishika nafasi ya pili mbele ya Hamilton aliyekamata nafasi ya tatu.

Dereva kinda wa Ferrari, Charles Leclerc amemaliza kwenye nafasi ya sita ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kushinda mara mbili mfululizo kwenye Belgian GP na Italian GP. 

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya