Formula 1: Nini Kinafuata Baada Ya Lewis Hamilton Kushinda Taji La Sita?

5th November 2019

MIAMI, Marekani- Usiku wa kuamkia jana, dereva nguli wa kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton alifanikiwa kushinda taji lake la sita la dunia.

Lewis Hamilton
Lewis Hamilton
SUMMARY

Hata hivyo wastani wa Hamilton kwenye hizo mbio ni mzuri kuliko wa Schumacher. Hamilton ana wastani wa kushinda mbio 10 kila msimu na kama ataendelea na wastani huo hadi msimu ujao basi itakuwa amefanikiwa kumzidi Schumacher.

Idadi hiyo imempeleka Hamilton hatua moja nyumba ya Michael Schumacher ambaye ameshinda mataji saba na akihesabika kama ni mwamba wa muda muda wote (G.O.A.T) wa mchezo wa mbio za magari.

Ni wazi kabisa kwasasa ni suala la muda tu kabla ya Hamilton kuweza kufikia idadi hiyo ya mataji na pengine hata kuipita na kuweka rekodi yake ya dunia.

Schumacher yeye alishastaafu mara baada ya kupata ajali mbaya iliyomfanya kuishi kwenye koma tangu mwaka 2012.

Kwahiyo Hamilton ndiye mtu anayeonekana kuwa karibu zaidi kufikia mafanikio hayo. Mwengine ambaye angeweza kufika huko ni Sebastian Vettel ambaye anashikilia mataji manne.

Lakini uwezo wa Mjerumani huyo kwa misimu ya hivi karibuni umekua si wa kuridhisha kiasi kwamba msimu huu ameshinda kwenye mbio moja tu kati ya 19 za msimu.

Msimu huu bado kuna mbio mbili zimebaki ambazo ni Brazil GP na Abu Dhabi GP. Mashindano hayo yalioyobaki yatakuwa ni ya kukamilisha tu ratiba za msimu huu wa Formula 1.

Hata hivyo licha ya kuwa ni mbio za kukamilisha ratiba lakini kwa upande mwingine bado zina umuhimu hasa kwa Hamilton ambaye anapigania nafasi ya kuwa gwiji wa mchezo huo akimshusha Schumacher ambaye amekaa hapo kwa muda mrefu.

Hamilton ndiye anaonekana kuwa ni mpinzani wa kweli wa Schumacher kwenye hadhi hiyo ya kuwa miongoni mwa magwiji wa mchezo huo lakini ni takwimu gani nyingine ambazo Muingereza huyo zina mfananisha na Schumacher?

-Hamilton kwasasa ni mchezaji wa pili kuwa na mafanikio zaidi nyuma ya Schumacher. Hamilton ana mataji 6 wakati Schumacher ana mataji 7.

-Taji la sita aliloshinda msimu huu ina maana kuwa Hamilton amemfunika gwiji wa Argentina, Juan Manuel Fangio. Fangio alishinda mataji matano kwenye miaka ya 1950.

-Huu ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Hamilton ambaye ameshinda (2017, 2018, 2019). Record ya kushinda mataji mengi mfululizo anaishikilia Michael Schumacher ambaye alishinda kuanzia mwaka 2000 hadi 2004.

-Hata hivyo huu ni ushindi wa tano kati ya misimu sita iliyopita. Utawala wa Hamilton ndani ya misimu sita iliyopita uliingiliwa na dereva mwenzake wa Mercedes, Nico Rosberg ambaye alinyakuwa taji mwaka 2016.

-Dereva pekee ambaye hadi hivi sasa bado anashindana na amewahi kushinda ubingwa zaidi ya mara moja ni Sebastina Vettel ambaye ana mataji manne.

-Hamilton ameshinda kwenye mbio tofauti 83 akiwa nyuma ya Schumacher ambaye ameshinda mara 91, Vettel yeye ameshinda mara 53.

-Hata hivyo wastani wa Hamilton kwenye hizo mbio ni mzuri kuliko wa Schumacher. Hamilton ana wastani wa kushinda mbio 10 kila msimu na kama ataendelea na wastani huo hadi msimu ujao basi itakuwa amefanikiwa kumzidi Schumacher.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya