Formula 1: Lewis Hamilton Atoa Lake La Moyoni Kuhusu Kampuni Ya Ferrari

24th September 2019

SINGAPOO, Singapore -Bingwa wa zamani wa mbio za magari wa kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton amesema ni ngumu sana kwasasa kushindana na madereva wa kampuni ya Ferrari kutokana na ubora wao unaosababishwa na aina ya magari wanayotumia.

Lewis Hamilton
Lewis Hamilton
SUMMARY

"Sio kama hatujawahi kushindana na gari za aina hii, hapana, tulishindana nazo huko nyuma na tuaweza kufanya vizuri ila niseme tu sio kazi ndogo hata kidogo,"


SINGAPOO, Singapore -Bingwa wa zamani wa mbio za magari wa kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton amesema ni ngumu sana kwa sasa kushindana na madereva wa kampuni ya Ferrari kutokana na ubora wao unaosababishwa na aina ya magari wanayotumia.

Hamilton ameyasema hayo ikiwa ni siku moja tu kupita tangu madereva wa Ferrari walipomenyana vikali kushindani taji la Singapore GP ambapo Sebastian Vettel aliibuka mshindi huku dereva mwenzie Charles Leclerc akishika nafasi ya pili.

"Kampuni ya Ferreari kwasasa ina magari mazuri ambayo yatatusumbua sana kwa msimu huu, nadhani ni kitu kigumu kwasasa kuweza kuwashusha wale jamaa," amesema Hamilton ambaye alimaliza nafasi ya nne kwenye Singapore GP.

"Sio kama hatujawahi kushindana na gari za aina hii, hapana, tulishindana nazo huko nyuma na tuaweza kufanya vizuri ila niseme tu sio kazi ndogo hata kidogo,"

Ushindi wa Vettel siku ya Jumapili umekuwa ni wa tatu mfululizo kwa kampuni ya Ferrari ambayo pia waliibuka kidedea kwenye Belgium GP na Italian GP ambazo zote zilinyakuliwa na bwana mdogo machachari Leclerc ambaye amejiunga na Ferrari msimu huu.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya