Formula 1: Lewis Hamilton Atangaza Nia Ya Kuendelea Kudumu Ndani Ya "Game"

15th November 2019

LONDON, Uingereza- Bingwa mara sita wa mashindano ya Formula 1, Lewis Hamilton ameweka wazi kuwa bado ana nia ya kuendelea kushiriki michuano hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Lewis Hamilton
Lewis Hamilton
SUMMARY

Hamilton, 34 ana mkataba na kampuni ya Mercedes ambao unaisha mwishoni wa msimu wa 2020 lakini amesema kuwa anatarajia kuongeza tena.

LONDON, Uingereza- Bingwa mara sita wa mashindano ya Formula 1, Lewis Hamilton ameweka wazi kuwa bado ana nia ya kuendelea kushiriki michuano hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Hamilton, 34 ana mkataba na kampuni ya Mercedes ambao unaisha mwishoni wa msimu wa 2020 lakini amesema kuwa anatarajia kuongeza tena.

Inatambulika kuwa kwasasa mazungumzo ya kumuongezea mkataba ndani ya Mercedes yamefika pazuri na yeye mwenyewe ameonesha nia ya kutaka kuendelea kubakia hapo.

Hata hivyo hofu pekee iliyo kwasasa ni kuhusu maisha ya Toto Wolf bosi wa Merdcedes ambaye inasemekana huenda akaondoka kwenye timu hiyo na kwenda kufanya kazi ndani ya Formula 1.

Wolf ambaye tangu alipojiunga na Mercedes mwaka 2013 hakuwa kukosekana kwenye michuano yoyote ile kwa mara ya kwanza atakosekana kwenye Brazil GP ambayo inatarajia kuanza leo.

Mwenyewe Wolf amesema kuwa ni kwasababu ya majukumu mengine lakini taarifa za kutoka vyanzo tofauti zinasema kuwa huenda ana mpango wa kuondoka.

Mercedes pamoja na Hamilton wote tayari wameshashinda taji la msimu huu na sasa wana mbio mbili mbele yaani hizi za Brazil na zile za Abu Dhabi GP ili kukamilisha msimu.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya