Formula 1: Lewis Hamilton Atamani Kufanya Kazi Na Sebastian Vettel

5th October 2019

LONDON, Uingereza- Bingwa wa michuano ya mbio za magari, Lewis Hamilton amesema kuwa anafaa kufanya kazi ndani ya Ferrari.

Lewis Hamilton
Lewis Hamilton
SUMMARY

Hamilton baada ya ushindi kwenye Russian GP wiki iliyopita anatarajia kuingia tena vitani kuwania Japan GP inayotarajia kuanza wiki ijayo ambapo kama kawaida itambidi kukabiliana vikali na madereva wawili wa Ferrari ambao ni Vettel na bwana mdogo Charles Leclerc.

Hamilton ambaye yupo chini ya kampuni ya Mercedez tangu akiwa na miaka 13 amesema hayo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha runinga nchini Uingereza.

Ferrari ni kampuni pinzani ya Mercedez ambayo ndani yake yupo mkali Sebastian Vettel na kama wazo la Hamilton litatimia basi mahasimu hao watafanya kazi ndani ya kampuni moja.

"Kwa jinsi ninavyojiona ninafaa kufaa nguo nyekundu (akimaanisha sare za Ferrari), hata hivyo bado ni kitendo kigumu sana ukizingatia nimefanya kazi ndani ya Mercedez tangu nikiwa nina umri wa miaka 13," amesema Hamilton.

Hamilton baada ya ushindi kwenye Russian GP wiki iliyopita anatarajia kuingia tena vitani kuwania Japan GP inayotarajia kuanza wiki ijayo ambapo kama kawaida itambidi kukabiliana vikali na madereva wawili wa Ferrari ambao ni Vettel na bwana mdogo Charles Leclerc.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya