Formula 1: Lewis Hamilton Ambwaga Sebastian Vettel Na Kutwaa Ubingwa Wa Mexico GP

28th October 2019

MEXICO CITY, Mexico- Lewis Hamilton ameshinda Mexico GP baada ya kuwadhibiti vizuri wapinzani wake kutoka kampuni ya Ferrari hasa Sebastian Vettel ambaye alionesha kuwa ni kikwazo kwake kwenye mbio hizo.

Lewis Hamilton
Lewis Hamilton
SUMMARY

Wanaume hao walikuwa karibu sawa kwa kila kitu kwenye mzunguko wa mwisho lakini Hamilton akatumia akili yake ya kuzaliwa na uzoefu wake kuhakikisha anamaliza akiwa kinara.

Hata hivyo licha ya ushindi huo lakini Hamilton atalazimika kusubiri hadi Jumapili ijayo kwenye US GP kunyakuwa taji lake binafsi kwa mara ya sita lakini hiyo ni endapo hatodondosha alama 22 dhidi ya mpinzani wake wa ndani ya Mercedes, Valetteri Bottas.

Hamilton ameshinda kwenye msuguano mkali wa madereva wa tatu ambao ni Vettel na Charles Leclerc wa Ferrari pia Bottas ambaye ni wa kutoka kampuni ya Mercedes.

Wanaume hao walikuwa karibu sawa kwa kila kitu kwenye mzunguko wa mwisho lakini Hamilton akatumia akili yake ya kuzaliwa na uzoefu wake kuhakikisha anamaliza akiwa kinara.

Kwenye mbio hizo, Vettel alimaliza kwenye nafasi ya pili huku Bottas akishika namba tatu na Leclerc akasalia kwenye nafasi ya nne.

"Tumekuja hapa tukidhani kuwa tuna nafasi ngumu ya kushinda lakini tumeshinda, nilipata majeraha kidogo hivyo niliendelea lakini kwa ugumu sana, hata hivyo kitu kikubwa ni kwamba tumeendelea kujijengea heshima," amesema Hamilton.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya