Formula 1: Japan GP Yasitisha Shughuli Zake Za Jumamosi Kupisha Kimbunga

11th October 2019

TOKYO, Japan -Mamlaka zinazosimamia michuano ya mashindano ya magari Formula 1 wametangaza kughairisha shughuli zote za mchujo wa Japan GP zilizotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi kupisha kimbunga.

Formula 1
Formula 1
SUMMARY

Kwa mujibu wa mamlaka za hali ya hewa nchini Japan taarifa zinasema kuwa kimbunga hicho kitafuatiwa na upepo mkali Jumapili siku ambayo mashindano yamepangwa kufanyika.

Siku ya Jumamosi baadhi ya miji ndani ya Japan inatarajiwa kukumbwa na kimbunga kikali ambacho kinaweza kuzua taharuki kqwenye baadhi ya shughuli.

Kwa mujibu wa mamlaka za hali ya hewa nchini Japan taarifa zinasema kuwa kimbunga hicho kitafuatiwa na upepo mkali Jumapili siku ambayo mashindano yamepangwa kufanyika.

Taarifa iliyotoka jana (Alhamisi) kutoka Formula 1 ilieleza kuwa walitamani kila kitu kiendelee kama ilivyopangwa kwenye ratiba lakini usalama wa madereva na mashabiki ni kitu ambacho walikuwa wanakipa kipaumbele cha hali ya juu.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya