Formula 1: Japan GP Kumzalisha Nyota Mwingine Wa Mbio Za Magari Dunia

7th October 2019

TOKYO, Japan -Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya wapenzi wa mashindano ya magari kushuhudia kipute cha Japan GP, taarifa zimetoka zikisema kuwa kwenye mashindano hayo kutakuwa na jina jipya ambalo lituwa linashiriki kwa mara ya kwanza.

Naoki Yamamoto
Naoki Yamamoto
SUMMARY

Japan GP inatarajiwa kushika kasi siku ya Jumapili lakini kabla ya kufika huko kuna hatua za mchujo ambazo zitaisha siku ya Jumamosi.

Huyo si mwingine bali ni Mjapani, Naoki Yamamoto, 31, ambaye atashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza akiwa chini ya timu ya Toro Rosso ambayo ina ushirikiano na Honda.

Yamamoto ni bingwa mtetezi wa michuano ya magari inayoendeshwa nchini Japan ya Super Formula na Super GT.

Katika mashindano ya Super GT aliwahi kushirikiana na bingwa wa Formular 1, Jenson Button.

"Kushiriki Formula 1 ilikuwa ni ndoto yangu ya tangu utotoni ambayo sasa naona imetimia," amesema Yamamoto.

Japan GP inatarajiwa kushika kasi siku ya Jumapili lakini kabla ya kufika huko kuna hatua za mchujo ambazo zitaisha siku ya Jumamosi.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya