Formula 1: Bifu Jipya Lazuka Ndani Ya Ferrari, Sebastian Vettel Akifuta Ukame Wa Mataji

23rd September 2019

Bingwa wa zamani wa magari yaendayokasi, Sebastian Vettel ameshinda ubingwa wa mbio za Singapore Grand Prix mbele ya dereva mwenzie wa kampuni ya Ferrari, Charles Leclerc na kufuta ukame wake wa miezi 13 bila kushinda taji lolote.

Singapore Grand Prix
Singapore Grand Prix
SUMMARY

Vettel alianza shindano akiwa nafasi ya tatu lakini alipambana kwenda kukaa mbele ya dereva mwenzake wa Ferrari, Leclerc ambapo baada ya kufanikiwa kumuweka nyuma basi alimdhibiti kuhakikisha kuwa hatoki huko nyuma hadi mizunguko yote itakapokwisha.

Bingwa wa zamani wa magari yaendayokasi, Sebastian Vettel ameshinda ubingwa wa mbio za Singapore Grand Prix mbele ya dereva mwenzie wa kampuni ya Ferrari, Charles Leclerc na kufuta ukame wake wa miezi 13 bila kushinda taji lolote.

Hata hivyo ushindi huo haujapokelewa kwa furaha na Leclerc ambaye anahisi alichezewa figisu na akasema kwamba anahisi suala hilo linaweza kuzalisha bifu ndani ya timu yao wenyewe.

Yote kwa yote, ushindi huo umekuwa ni muhimu zaidi kwa Vettel ambaye ni bingwa mara nne wa michuano ya dunia.

Msimu huu ulikuwa ni mgumu sana kwake kiasi cha kwamba watu walinza kuhoji kuhusu uwezo wake na pengine kuhusu nini kinafuata katika maisha yake ndani ya Formula 1.

Vettel raia wa Ujerumani amekuwa akitoa maboko kwenye kila mashindano ambayo yamekuwa yakimgharimu kitu kilichotoa nafasi kwa Leclerc kuibuka kuwa mtu muhimu ndani ya timu ya Ferrari akifanikiwa kushinda mataji mawili ndani ya msimu wake wa kwanza kwenye kampuni hiyo.

Vettel Amefanya Figisu Gani?

Vettel alianza shindano akiwa nafasi ya tatu lakini alipambana kwenda kukaa mbele ya dereva mwenzake wa Ferrari, Leclerc ambapo baada ya kufanikiwa kumuweka nyuma basi alimdhibiti kuhakikisha kuwa hatoki huko nyuma hadi mizunguko yote itakapokwisha.

"What the hell," alisikika Leclerc kwenye redio yake ya ndani ya gari wakati mashindano yakiendela akihoji baada ya kuona anafanyiwa figisu na dereva ambaye anatoka naye kwenye kampuni moja.

"Ni bora niwaeleze ukweli vile ninajihisi, kiukweli nimeumia sana, sielewi kwanini imekuwa hivi lakini nadhani tutajadili baadaye," amesema Leclerc alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari baada ya shindano kuisha.

Lewis Hamilton Maji Ya Shingo

Wakati mafahari wawili ndani ya Ferrari wakizozana kuhusu nafasi ya kwanza na ya pili, bingwa wa zamani wa michuano hiyo, Lewis Hamilton aliye ndani ya kampuni ya Mercedes amejikuta akimaliza kwenye nafasi ya nne nyuma ya Max Verstappen wa kampuni ya Red Bull aliyeshika nafasi ya tatu.

Hamilton alikaa kwenye nafasi ya pili kwa mizunguko mingi lakini alijikuta akizamishwa hadi nafasi ya nne licha ya kuwa hakufanya mabadiliko ya matairi mara kwa mara.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya