Fomular 1: Vibweka Vyatawala Max Verstappen Akishinda Brazilian GP

18th November 2019

SAO PAULO, Brazil -Dereva wa Red Bull, Max Verstappen ameshinda mbio za Brazil GP kwa mtindo wa aina yake baada ya vibweka vingi kutawala kwenye shindano hilo lililofanyika Jumapili usiku.

Max Verstappen
Max Verstappen
SUMMARY

Hata hivyo maswali ya wapenda mchezo huu yatakuwa ni kujiuliza juu ya Vettel ambaye kwa tabia zake za hivi karibuni ameonekana kuwa na vita ya ndani kwa ndani dhidi ya dereva mwenzake ndani ya Ferrari, Leclerc.

Wakati Verstappen anashinda nyuma yake kulikuwa na drama nyingi ikiwemo ya madereva wa Ferrari, Sebastian Vettel na Charles Leclerc kugongana wakati wakiwa wanagombea nafasi ya nne.

Mbali na ajali ya madereva wa Ferrari lakini pia bingwa wa mwaka huu dereva wa Mercedes, Lewis Hamilton alijikuta akigonga na dereva mwingine wa Red Bull Alexander Albon kitu ambacho kilisababisha dereva wa Toro Rosso, Pierre Gasly kumaliza akiwa nafasi ya pili.

"Ilikuwa ni moja kati ya mbio bora kabisa za msimu huu ambazo zilikusanya matukio mengi katikati ya mashindano na hivyo nashukuru kuweza kuibuka mshindi," amesema Verstappen mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo.

Verstappen alistahili ushindi huo kwenye mbio ambazo alizitawala kuanza mwanzo kabisa wa mchezo lakini Gasly unaweza kusema kuwa alikuwa ni nyota wa mchezo. 

Hamilton na timu yake ya Mercedes licha ya kuwa tayari wameshabeba mataji yote ya msimu huu lakini walikutana na wakati mgumu sana kwenye mbio hizi.

Hata hivyo maswali ya wapenda mchezo huu yatakuwa ni kujiuliza juu ya Vettel ambaye kwa tabia zake za hivi karibuni ameonekana kuwa na vita ya ndani kwa ndani dhidi ya dereva mwenzake ndani ya Ferrari, Leclerc.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya