Fomular 1: Msimu Wa Mbio Za Magari Unafungwa Leo Kwenye Abu Dhabi GP

1st December 2019

ABU DHABI, UAE- Msimu wa Fomular 1 unatarajia kufungwa leo huko kwenye nchi za Falme za Kiarabu kwenye Abu Dhabi GP ambpo tayari Kampuni ya Mercedes pamoja na dereva wao Lewis Hamilton wameshatawa mataji mapema.

Formula 1
Formula 1
SUMMARY

Hamilton licha ya kushinda taji tangu kwenye US GP lakini bado ameendelea kusisitiza kuwa anataka kushinda zaidi kwenye mbio zilizobaki ikiwemo hii ya Abu Dhabi inayofanyika leo.

Mbio hizi zilizobaki ni za kukamilisha ratiba kama utazichukulia hivyo lakini kwa wenyewe madereva na viongozi wa makampuni yanayoshindana huzichukukulia mbio hizo kama sehemu ya kuendelea kuboresha rekodi zao mbalimbali.

Hamilton licha ya kushinda taji tangu kwenye US GP lakini bado ameendelea kusisitiza kuwa anataka kushinda zaidi kwenye mbio zilizobaki ikiwemo hii ya Abu Dhabi inayofanyika leo.

Na kwa kuonesha kuwa ni kweli anachosema ana maanisha leo jana amemaliza kwa kishindo katika majaribio yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Ijumaa ambapo ameibuka kwenye nafasi ya kwanza.

Kwenye msimamo wa madereva 20, Hamilton anaongoza akiwa na alama 387 baada ya kushinda kwenye mbio 10 tofauti.

Dereva mwenzake kutoka Mercedes, Valteri Bottas anafuatia kwenye nafasi ya pili akiwa na alama 314 baada ya kushinda kwenye mbio 4.

Max Versterppen wa Red Bull yeye yupo nafasi ya tatu kwenye msimamo akiwa na alama 260 huku akiwa ameshinda mbio 3.

Madereva wa Ferrari, Charles Leclerc na Sebastian Vettel wamefuatana kwenye nafasi ya nne na ya tano.

Leclerc yupo namba nne akiwa ameshinda mbio 2 na anajumla ya pointi 249, wakati Vettel yeye anashikilia namba 5 akiwa ameshinda mbio moja tu msimu huu na ana alama 230.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya