Fomular 1: Hamilton Aikaribia Rekodi Ya Schumacher Baada Ya Kushinda Taji La Dunia

4th November 2019

MIAMI, Marekani- Lewis Hamilton ameshinda taji la sita la dunia baada ya kumaliza michuano ya USA GP akiwa kwenye nafasi ya pili nyuma ya derecva mwenzake wa Mercedes, Valtteri Bottas.

Lewis Hamilton
Lewis Hamilton
SUMMARY

Kwa madereva ambao wapo hadi hivi sasa na wakiwa na mataji mengi ni Sebastian Vettel wa Ferrari mwenye mataji manne ambaye ndiye anaweza kuwa tishio kwa Hamilton kwa siku za usoni.

Ushindi huo unamaanisha kuwa Hamilton sasa yupo hatua moja nyuma ya Michael Schumacher anayeshikilia rekodi ya dunia akiwa na mataji saba.

Hamilton alijaribu kwa kila namna kutaka kumaliza akiwa nafasi ya kwanza kwenye US GP iliyofanyika usiku wa kuamkia leo lakini alijikuta akizidiwa mbinu na dereva mwenzie wa Mercedes, Bottas ambaye alifanikiwa kumaliza akiwa kinara.

Hata hivyo hiyo haikuwa kiwakozo kwake kwani alichokuwa anatakiwa kufanya jana Hamilton ni kumaliza akiwa ndani ya nane bora tu ili aweze kushinda taji lake la sita la dunia.

Nafasi ya tatu kwenye mbio hizo za Marekani imekwenda kwa dereva wa Red Bulls, Max Verstappen.

"Wakati nikiwa na umri wa miaka sita au saba, baba yangu alinifundisha kutokata tamaa, nilikuwa ninaamini nitashinda ingawa nilikuwa najua kuwa ni ngumu sana," amesema Hamilton.

Hamilton ameshinda taji hilo baada ya kushinda kwenye mbio 10 kati ya 19 za msimu huu huku ikiwa bado kuna mbio mbili zimebaki Brazil GP na Abu Dhabi GP.

Kwa madereva ambao wapo hadi hivi sasa na wakiwa na mataji mengi ni Sebastian Vettel wa Ferrari mwenye mataji manne ambaye ndiye anaweza kuwa tishio kwa Hamilton kwa siku za usoni.

Orodha Kamili Ya Mabingwa Wa Dunia:

Michael Schumacher 7 (Amestaafu)

Lewis Hamilton 6 (Bado Yupo)

Juan Manuel Fangio 5 (Amestaafu)

Alain Prost 4 (Amestaafu)

Sebastin Vettel 4 (Bado Yupo)

Jack Brabham 3 (Amestaafu)

Jackie Stewart 3 (Amestaafu)

Niki Lauda 3 (Amestaafu)

Nelson Piquet 3 (Amestaafu)

Ayrton Senna 3 (Amestaafu)

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya