Fomular 1: Charles Leclerc Amtupia Lawama Vettel Kufuatia Ajali Ya Brazilian GP

29th November 2019

ABU DHABI, UAE- Dereva wa kampuni ya Ferrari, Charles Leclerc amesema kuwa Sebastian Vettel alikuwa anajua jinsi ya kuiepusha ajali iliyotokea kwenye Brazilian GP lakini hakuamua kufanya hivyo.

Charles Leclerc
Charles Leclerc
SUMMARY

Wiki mbili zilizopita, madereva wawili wa Ferrari, Sebastian Vettel na Charles Leclerc wakati wakishiriki Brazilian GP walijikuta wamegongana na kusababisha ajali kubwa iliyopelekea wao kushindwa kufanya vizuri kwenye mbio hizo.

Leclerc anasema kwa upande wake yeye alijitahidi sana kukwepa ajali ile na ndiyo maana alikimbilia upande wa kushoto hivyo ilikuwa ni kazi ya Vettel kutokwenda upande ule lakini jamaa aliamua kumfuata na hatimaye ajali ikatokea.

Hata hivyo Leclerc amesema kuwa baada ya kikao chao cha ndani kwasasa hakuna tatizo na sasa wanajiandaa na mbio za kufungia msimu huu ambazo zitafanyika Abu Dhabi kwenye wikiendi hii.

"Vettel hakupaswa kunifuata mimi kwenye upande wa kushoto na hilo yeye analijua vizuri, mimi nilifanya kazi kubwa ya kuhakikisha tunaepusha ajali"

"Kitu cha muhimu kwasasa ni kwamba kila kitu kipo sawa na tunasonga mbele," amesema Leclerc wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.

Leclerc ameongeza kwa kusema kuwa kwasasa hawataweza kukamiana baada ya kikao chao cha ndani kilichofanyika chini ya bosi wao Matiia Binotto siku chache kabla ya Abu Dhabi GP.

Kwani Ilikuwaje? 

Wiki mbili zilizopita, madereva wawili wa Ferrari, Sebastian Vettel na Charles Leclerc wakati wakishiriki Brazilian GP walijikuta wamegongana na kusababisha ajali kubwa iliyopelekea wao kushindwa kufanya vizuri kwenye mbio hizo.

Ajal yao ilitoa mwanya kwa wapinzani wao kushinda ambapo, Max Verstappen wa Red Bull kuibuka kidedea kwenye mbio hizo.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya