European Open: Andy Murray Asonga Mbele, Cameroon Norrie Akwama Mbele Ya Lopez

16th October 2019

Bingwa wa zamani wa dunia wa mchezo wa tenesi, Andy Murray amesonga mbele kwenye michuano ya European Open baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Mbelgiji, Kimmer Coppejans.

Andy Murray
Andy Murray
SUMMARY

Kutokana na matokeo hayo, Murray sasa atakutana na mchezaji namba nane kwa ubora Pablo Cuevas wa Uruguay au Mbolivia, Hugo Dellien kwenye hatua ya 16 bora itakayoanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii.

Murray raia wa Uingereza ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amepungua ubora kutokana na majeraha ya paja ameshinda kwa jumla ya seti  6-4 7-6 (7-4) dhidi ya mpinzani wake huyo anayeshika nafasi ya 158 kwa ubora duniani.

Kutokana na matokeo hayo, Murray sasa atakutana na mchezaji namba nane kwa ubora Pablo Cuevas wa Uruguay au Mbolivia, Hugo Dellien kwenye hatua ya 16 bora itakayoanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii.

Kwa upande wake Cameroon Norrie yeye amekumbana na kipigo kutoka kwa Mhispania, Feleciano Lopez na kutupwa nje ya mashindano hayo.

Norrie 24, raia wa Uingereza amefungwa kwa jumla ya seti 7-6 (7-2) 6-4 dhidi ya Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 38.

Licha ya kufungwa huko lakini Norrie anatarajiwa kutangazwa kuwa mchezaji namba mbili kwa ubora nchini Uingereza nyuma ya Dan Evans ambaye amemshusha Kyle Edmund kwenye nafasi ya kwanza.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya