Europa Haipoi Wala Haiboi; Haya Ndiyo Mambo Makubwa Matano Yaliyojiri Mzunguko Wa Nne

8th November 2019

MANCHESTER, Uingereza- Michuano ya Europa iliendelea kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo ambapo miamba mbalimbali ilikuwa viwanjani kusaka matokeo.

Mason Greenwood
Mason Greenwood
SUMMARY

Sare ya 1-1 waliyopta Arsenal dhidi ya Vitoria ni ya nne mfululizo kwa timu hiyo kwenye michuano yote. Kibaya zaidi ni kwamba kwenye michezo yote hiyo ambaye wamepata sare wao ndio walikuwa wanaongoza kabla ya wapinzani kuchomoa.

Yafuatayo ni makubwa kwa uchache ambayo yamejiri kwenye michuano hiyo kama yalivyoandaliwa na SportPesa News.

Mason Greenwood Aisongesha Man United

Manchester United wamekuwa ni miongoni mwa timu chache ambazo zimefanikiwa kufuzu hatua ya 32 bora baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Partizina Belgrade.

Hata hivyo kwenye mchezo huo kinda wa timu ya Man United, Mason Greenwood amezidi kuonesha kuwa yeye ni mchezaji wa aina gani baada ya kufunga bao safi sana pamoja na kutengeza jingine ambalo limefungwa na Marcus Rashford.

Hilo ni bao la pili kwa Greenwood kwenye michuano hii msimu huu. Bao la kwanza alifunga kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Astana.

Arsenal Bado Wanasuasua

Sare ya 1-1 waliyopta Arsenal dhidi ya Vitoria ni ya nne mfululizo kwa timu hiyo kwenye michuano yote. Kibaya zaidi ni kwamba kwenye michezo yote hiyo ambaye wamepata sare wao ndio walikuwa wanaongoza kabla ya wapinzani kuchomoa.

Neil Lennon Awapaisha Celtic

Celtic wamewafunga Lazio nyumbani na ugenini. Mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita ndani ya uwanja wa Celtic Park, wenyeji walishinda 2-1 na jana tena wakiwa ugenini wameshinda kwa idadi hiyo.

Shukrani zote ni kwa kocha Neil Lennon ambaye anaonekana yupo vyema kimbinu na kuifanya Celtic ianze kuwa mwiba tena kwenye michezo ya ulaya. Tangu Celtic walivyowafunga Barcelona hawakuwa kurudi kwenye ubora kama huu waliokuwa nao sasa hivi.

Ushindi mfululizo waliopata kwenye mechi zao umewafanya nao kukata tiketi ya 32 bora mapema zikiwa zimesalia mechi mbili kwa kila timu.

Steven Gerald Hapoi Wala Haboi

Ushindi wa 2-0 walioupata Rangers dhidi ya FC Porto ni moja kati ya ushindi mkubwa aliowahi kupata Steven Gerald akiwa kama kocha wa kikosi hicho.

Baada ya mchezo huo, Gerald alimsifu sana mshambuliaji wake raia wa Colombia, Alfredo Morelos ambaye alikuwa mfungaji wa bao la kwanza kwenye mchezo huo kwa kusema kuwa anafurahi sana kufanya kazi na mchezaji huyo.

Wolves waibuka Jioni Tena

Kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza ugenini, Raul Jimenez amefunga tena bao la jioni na kuipa tena ushindi wa 1-0 timu yake ya Wolves mbele ya Slovan Bratislava.

Ushindi huo ni wa pili kwa Wolves ambao kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita, Wolves walishinda 2-1 muuaji akiwa ni Jimenez tena.

Imeandaliwa na Jerru Mlosa