Euro 2020: Mechi Hizi Tano Za Kufuzu Euro 2020 Zitasimamisha Dunia

13th November 2019

INSTANBUL, Uturuki -Ligi zote barani ulaya zimesimama na sasa macho yetu yote yatakuwa sehemu moja tu kwenye mechi za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2020.

Van Dijk  na De ligt
Van Dijk na De ligt
SUMMARY

Kwenye mechi kati ya Northen Ireland dhidi ya Uholanzi anahitajika mshidi ili walau kulipa sura kundi hili, la sivyo kundi litakuwa gumu hadi siku ya mwisho na huenda tukamkosa kigogo mmoja. Kwahiyo mechi hii itaweza kutoa walau majibu kiasi fulani.

INSTANBUL, Uturuki -Ligi zote barani ulaya zimesimama na sasa macho yetu yote yatakuwa sehemu moja tu kwenye mechi za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2020.

Wiki hii kunapigwa mechi kali sana au unaweza kuziita mechi za roho mbaya na hata kidogo usithubutu kusema kwamba wikiendi itapooza.

Timu zote kubwa zitakuwa viwanjani zikiwa sambaamba na nyota wao ambao wamekuwa wakiwasha moto kwenye vilabu mbalimbali.

Nafasi zinazowaniwa ni mbili tu kutoka kila kundi kwa timu kukata tiketi ya moja kwa moja kushiriki Euro 2020. Zipo nafasi chache kwa ajili ya play offs lakini mara nyingi timu nyingi huwa zinapenda kumaliza kazi mapema.

Kwasasa timu nyingi zimebakiwa na michezo miwili mkononi. Baadhi yao zimeshafuzu na kwenye wiki hii itakuwa ni bata tu. Pia kuna nyingine zina uhakika zitafuzu kwenye wiki hii na hivyo kumaliza kazi mapema.

Hata hivyo kuna makundi bado watu wameshikana nganganga na kufanya michezo hii ya mwishoni kuwa ni mikali na ya kusisimua zaidi kuitazama.

SportPesa News inakuletea mechi kali ambazo zitasimamisha watu mamilioni kwa mamilioni ndani ya dakika 90 za mchezo.

Uturuki v Iceland (Nov 14)

Vinara wa kundi H timu ya taifa ya Uturuki leo watakuwa dimbani kuwakaribisha Iceland ambao wapo kwenye nafasi ya tatu.

Unajua utamu wa mechi hii upo wapi? Ngoja nikwambie. Uturuki wanaongoza kundi wakiwa na alama 19 chini yao wapo Ufaransa nao wana alama 19. Iceland kwenye nafasi ya tatu wana alama 15.

Endapo Uturuki watafungwa leo na Ufaransa watashinda au kutoka sare basi watashushushwa hadi nafasi ya pili na kufuzu kwao itategemea matokeo ya mchezo wa mwisho. Na kama Iceland watafungwa basi safari yao itakuwa imefika mwisho. Hivyo lazima lipigwe bonge moja la mechi.

Romania v Sweden (Nov 15)

Kwenye kundi F inapiganiwa nafasi moja ya kufuzu baada ya nafasi nyingine kuwa ipo tayari imeshachukuliwa na Hispania.

Timu zinazoshika nafasi ya pili na ya tatu ni Romania na Sweden ambao tofauti yao ni alama moja tu. Mshindi wa mechi ya hii atakuwa na nafasi kubwa ya kufuzu moja kwa moja kama pia atafanya vizuri kwenye mchezo wa mwisho mapema wiki ijayo.

Northern Ireland v Uholanzi (Nov 16)

timu tatu kutoka kwenye kundi C zote zinanafasi sawa ya kufuzu. Uholanzi wapo kileleni wakifuatiwa na Ujerumani na timu zote zina alama 15. Northern Ireland wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 12.

Kwenye mechi kati ya Northen Ireland dhidi ya Uholanzi anahitajika mshidi ili walau kulipa sura kundi hili, la sivyo kundi litakuwa gumu hadi siku ya mwisho na huenda tukamkosa kigogo mmoja. Kwahiyo mechi hii itaweza kutoa walau majibu kiasi fulani.

Ujerumani v Northern Ireland (Nov 19)

Kama iliovyo kwenye mechi ya juu na mechi hii ndiyo mule mule. Northern Ireland anatakiwa kupigana kufa au kupona kwenye mechi mbili hizi la sivyo safari yake itaishia hapa.

Na kama watafanikiwa kusumbua mahakama basi kuna kigogo pengine atakosa nafasi mbili za juu.

Irelan v Denmark

Hii ni fainali ndogo katia Kundi D kwasababu Ireland na Denmark wanalingana alama wote wakiwa na 12 huku Switzerland wakiwa nafasi ya tatu na alama zao 11.

Matokeo yoyeto kwenye mechi hii yatawanufaisha zaidi Uswizi ambao wao watakuwa na kibarua kingine dhidi ya Georgia na endapo wakishinda basi watakuwa kwenye nafas mbili za juu.

Imeandaliwa na Jerry Mlosa