EURO 2020: Toni Kroos Awapeleka Wajerumani Euro, Uhalanzi Nao Wapenya

17th November 2019

MUNICH, Ujerumani- Mabao mawili aliyofunga kiungo wa Ujerumani, Toni Kroos yameihakikishia timu yake kumaliza kama vinara wa kundi C wa wa kundi lao na kufuzu kwenye michuano ya Euro 2020 baada ya kuibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Belarus.

Toni Kroos
Toni Kroos
SUMMARY

Kroos ambaye anacheza klabu ya Real Madrid alifunga mabao yake kwenye dakika ya 55 na 83 na kufanya ushindi huo kuwa ni wa bila mashaka.

Kwenye mchezo huo Matthias Ginter alianza kuandika bao kwa upande wa Ujerumano kabla ya leon Goretzka kuongeza la pili dakika chache tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Kroos ambaye anacheza klabu ya Real Madrid alifunga mabao yake kwenye dakika ya 55 na 83 na kufanya ushindi huo kuwa ni wa bila mashaka.

Uholanzi Wapenya

Kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo ambao matokeo yake yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu tumeshuhudia timu ya Northen Ireland ikibanwa mbavu nyumbani na kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Uholanzi.

Kwa matokeo hayo inamaanisha sasa Uholanzi nao wamekata tiketi ya Euro ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa tangu mara ya mwisho waliposhiriki kombe la dunia mwaka 2014.

Northen Ireland ambao walitoa changamoto kubwa sana kwa vigogo ndani ya kundi hilo sasa watalazimika kusubiri michezo ya mtoano (play offs) ili kuona kama wataweza kubahatika nafasi.

Croatia Nao Wamo

Ushindi wa 3-1 walioupata Croatia dhidi ya Slovakia umewafanya kupata tiketi ya kuongoza kundi E pamoja na kufuzu kwenye michuano ya Euro 2020.

Robert Bozenik alianza kufungua akaunti ya mabao kwa upande wa Slovakia lakini Nikola Vlasic aliweka mambo sawa kwa upande wa Croatia ambao ndiyo walikuwa wenyeji.

Mabao mawili kutoka kwa Bruno Petkovic na Ivan Perisci yalinogesha ushindi huo muhimu kwa wana fainali hao wa kombe la dunia msimu uliopita.

Endapo Wales watapata ushindi dhidi ya Hungary siku ya Jumanne basi watafuzu wakiwa kwenye nafasi ya pili.

Familia Ya Hazard Kiboko

Eden Hazard amefunga mabao mawili na Thorgan Hazard amefunga bao moja wakati wa mchezo wa kundi I na mabao hayo yameiwezesha timu yao ya taifa ya Ubelgiji kuibuka na ushindi wa 4-1 ugenini dhidi ya Urusi.

Bao lingine kwa upande wa Ubelgiji limefungwa na Romelu Lukaku huku Urusi wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Georgi Dzhikiya.

Matokeo Mengine

Cyprus 1-2 Scotland

Azerbaijan 0-2 Wales

Slovenua 1-0 Latvia

Urusi 1-4 Ubelgiji

San Marino 1-3 Kazakhstan

Ujerumani 4-0 Belarus

Northen Ireland 0-0 Uholanzi

Croatia 3-1 Slovakia

Austria 2-1 Northen Macedonia

Isreal 1-2 Paland

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya