EURO 2020: Teemu Pukki Aipeleka Finland Euro Kwa Mara Ya Kwanza Kwenye Historia

16th November 2019

HELSINKI, Finland -Mshambuliaji wa Norwich, Teemu Pukki amefunga mabao mawili kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Liechtenstein na kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu michuano ya Euro 2020 kwa mara ya kwanza kabisa kwenye historia ya taifa hilo.

Pukki
Pukki
SUMMARY

Mara baada ya kipyenga cha mwisho maelfu ya mashabiki waliokuwa uwanjani hapo waliruka viunzi na kujazana uwanjani kwa ajili ya kusherehekea ushindi huo mkubwa kwa timu yao ya taifa.


Finland wanakwenda Euro 2020 wakiwa washindi wa pili ndani ya kundi J ambalo linaongozwa na Italia waliofuzu tangu mwezi uliopita.

Mbali na Pukki, mchezaji mwingine aliyefunga bao kwenye mchezo huo wa kihistoria ni Jasse Tuominen na kuhitimisha safari ya ya miaka 32 ya kushindwa kufuzu kwenye michuano mikubwa aidha ya Euro au kombe la dunia.

Mara baada ya kipyenga cha mwisho maelfu ya mashabiki waliokuwa uwanjani hapo waliruka viunzi na kujazana uwanjani kwa ajili ya kusherehekea ushindi huo mkubwa kwa timu yao ya taifa.

Finland itakuwa ni moja kati ya nchi zenye idadi ndogo sana ya watu ambapo kwa mujibu ya sensa ya mwaka 2014, idadi yao kwa makadirio walikuwa ni watu milioni 5.5.

Santi Cazorla Afufuka

Baada ya kukumbwa na tatizo la majeraha akiwa na timu ya Arsenal hadi watu kuamini kuwa huenda asingecheza tena mpira, hatimaye kiungo fundi wa mpira Santi Cazorla amezaliwa upya naweza kusema hivyo.

Hiyo ni baada ya kurudi chini Hispania ambapo kwasasa anacheza kwenye klabu ya Villareal akiwa ameifungia mabao matano msimu huu.

Kiwango chake kimefanya ajumuishwe kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa siku za hivi karibu na usiku wa kuamkia leo amefunga bao lake la kwanza baada ya miaka minne. Bao lake la mwisho ndani ya timu ya taifa alifunga mwaka 2015 kwenye mchezo wa kirafiki kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Uingereza.

Cazorla amefunga bao hilo wakati timu yake ya taifa ya Hispania ikitoa somo kwa Malta wakiibuka na ushindi wa 7-0. 

Mabao mengine kwenye mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Alvaro Morata, Pau Torres, Pablo Sarabia, Dani Olmo, Gerald Moreno na Jesus Navas.

Matokeo Mengine Euro

Armenia 0-1 Ugiriki

Finland 3-0 Liechtenstein

Norway 4-0 Faroe Islands

Bos-Herve 0-3 Italia

Denmark 6-0 Gilbraltar

Switzerland 1-0 Georgia

Romania 0-2 Sweden

Hispania 7-0 Malta

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya