EURO 2020: Luxembourg Wameshikilia Tiketi Ya Ureno Kwenda Euro, Fuatilia Dondoo

17th November 2019

DUDELANGE, Luxembourg -Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 kwenye mchezo uliopita lakini leo Ureno ndiyo wanamchezo wa kufa au kupona pale watakaposhuka uwanja wa ugenini kupepetana dhidi ya Luxembourg

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo
SUMMARY

Endapo wakishindwa kupata alama tatu basi nafasi ya watakuwa wameiweka rehani mbele ya Serbia ambao nao leo wana mchezo wa nyumbani dhidi ya vinara wa kundi Ukraine

DUDELANGE, Luxembourg -Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 kwenye mchezo uliopita lakini leo Ureno ndiyo wanamchezo wa kufa au kupona pale watakaposhuka uwanja wa ugenini kupepetana dhidi ya Luxembourg kwenye mchezo wa kundi B.

Kutoka kwenye kundi hilo, Ukraine tayari wameshakata tiketi yao tangu mwezi uliopita kazi imebaki kwa timu mbili ambazo ni Ureno aliyekuwa kwenye nafasi ya pili na Serbia walio kwenye nafasi ya tatu ambapo kwenye msimamo wanatofautiana alama moja tu.

Ureno ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo wanahitajika kushinda kwa namna yeyote ile ili waweze kufuzu moja kwa moja kwenye Euro 2020. 

Endapo wakishindwa kupata alama tatu basi nafasi ya watakuwa wameiweka rehani mbele ya Serbia ambao nao leo wana mchezo wa nyumbani dhidi ya vinara wa kundi Ukraine. Mechi zote zitapigwa muda wa saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki.

Moja kati ya timu hizo ambayo itashindwa kufuzu kupitia leo basi itabidi wasubiri michezo ya ngumi jiwe (play offs) ambayo imekuwa na kawaida ya kutoa matokeo ya kushtusha sana.

Kitu ambacho Ureno wataingia kwa kujivunia nacho sana kwenye mchezo wa leo ni ile rekodi yao nzuri dhidi ya Luxembourg.

Kwenye michezo saba ambapo timu hizi zimecheza tangu mwaka 2004, Ureno wameshinda mechi zote tena kwa idadi kubwa ya mabao. Kwenye mechi zote hizo Luxembourg wamefunga bao moja tu ilikuwa mwaka 2012 ambapo walifungwa 2-1 ikiwa ndo mechi walioyokaza sana.

Uingereza Na Mchezo Wa 1001

Wakiwa tayari wameshafuzu kucheza Euro 2020 timu ya taifa ya Uingereza leo watakuwa ugenini kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Kosovo kwenye kukamlisha michezo ya kundi A.

Mchezo huo utakuwa ni wa 1001 kwa timu ya taifa ya wanaume tangu iundwe. Ushindi walioupata dhidi ya Montenegro ilikuwa pia ni sherehe ya kufikisha michezo 1000 kwenye historia yao.

Ushindi au sare utawahakikisha Uingereza kumaliza kwenye nafasi ya kwanza kabisa ya kundi hilo lakini Kosovo hawatazurika na matokeo yoyote yale kwakuwa wameshajihakikishia nafasi ya kucheza michezo ya mtoano (play offs).

Mchezo wa leo mashabiki wa timu ya taifa ya Uingereza watapata nafasi ya kumuona kiungo mshambuliaji wao Raheem Sterling kama vile kocha Gareth Southagate alivyothibitisha kuwa atamuanzisha.

Sterling ambaye anacheza kwenye klabu ya Manchester City alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Montenegro ambapo Uingereza walishinda 7-0 kwasababu ya sintofahamu iliyojitokeza kambini kati yake na mlinzi wa Liverpool, Joe Gomez ambao wote wamo ndani ya kikosi cha timu ya taifa kwasasa.

Mchezo wa leo utakuwa ni wa pili baina ya timu hizo kukutana kwenye historia. Mchezo wa kwanza walikutana kwenye kundi hili mapema mwezi Septemba ambapo Uingereza wakiwa nyumbani Wembley walishinda kwa mabao 5-3.

Mechi Nyingine Leo

Bulgaria v Czech

Kosovo v Uingereza

Luxembourg v Ureno

Serbia v Ukraine

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya